Trafiki uliyopo tazara leo,hiyo adhabu uliyotoa ni kiboko!!

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,341
13,325
ama kweli leo,ndio nimekubali kuwa samaki mmoja akioza wote lazima waoze,leo ktk makutano ya barabara ya mandela na nyerere(tazara)kuna trafiki wa kike yuko pale,ameamua kutoruhusu magari yanayotoka mandera road kwenda buguruni/nyerere road,kwa takribani saa 1!kisa kuna dreva wa daladala alimpigia honi kuashiria mbona upande wao ameusahau!kweli dada akafunga vioo,tumekaa kwenye foleni,huku magari ya pande nyingine yanaruhusiwa bila shida!sasa pale amemkomoa dreva wa daladala yule au wote tuliokuwa kwenye foleni ile!mi nadhani bora wa ache tu taa zifanye kazi yake,hasa kipindi hiki cha mchana.
 
inawezekana kulikuwa na msafara maana kama ni honi washapigiwa sana, na saa nzima mkuu is quite long hata incharge wake huyo dada (huwa anasimama ng'ambo pale kwa kona karibia na ukuta opp na bakhresa) angenote na kuingilia kati
 
trafiki ni kama wana mapepo jua kali lote lile wanakomaa kuomgoza magari, si waache taa zifanye kazi? Nahisi kuna uchawi wanaufanya sioni mantiki kabisa jua kali vile trafiki yuko kwenye taa anaongoza gari. Na ukweli kuwa siku wasipoongoza magari hapo Tazara kuna hakuna foleni kabisa
 
tatizo hilo pale tazara lipo sana wanatoa priority kwa nyerere road zaidi ya mandela rd...na ukizingatia mandela rd ina matruck mengi basi kipande cha kutoka veternary hadi bakhresa kutumia one hour ishakuwa kawaida
 
Back
Top Bottom