Trafiki na ubambikaji wa makosa ya barabarani

Trafiki na ubambikaji wa makosa ya barabarani

darthvader

Member
Joined
Mar 17, 2018
Posts
77
Reaction score
64

Aiseee mbali na kuvunjika mbavu baada ya kuona hilo karagosi kuhusu vituko vya trafiki bongo imenifanya nitafakari kuhusu mamlaka yao yalivyo makubwa sasa hivi na wanavyoweza kukubambikia faini zaidi ya kosa ulilolifanya. Wiki kama mbili zimepita nilikamatwa maeneo ya Tangibovu kosa likiwa ni overspeeding, kwa kuwa ni mgeni maeneo hayo na kuna kibao cha hamsini nilitaka nieleweshwe maana nimeendesha chini ya 50kph.

Walinifahamisha kuwa kuna ujenzi wa daraja na kuna kibao cha mbao cha speed limit kiko chini na kinaonesha 30kph nilitakiwa nikione wakati nakuja. Baada ya kufokewa na askari mama mtu mzima waliyekuwa wanamuita matron nilikubali kuandikiwa fine kwa mbinde maana hoja yangu ilikuwa kibao kimewekwa chini tena cha mbao bila hata mlingoti dereva atakiona vipi kwa mbali hasa kama anaendesha kushoto mwa barabara. Maana kibao kiko eneo la katikati ya barabara na barabara.

Shida imekuja nimeenda kulipa Oysterbay police nakuta fine nayodaiwa ni Tshs 60,000 (yani makosa mawili) na si Tshs 30,000 niliyopewa tiketi. Ina maana niliongezewa kosa nisilo lifahamu. Nimelalamika mpaka kwa mkuu wao hakukuwa na msaada wowote zaidi ya kuambiwa nilipe maana deni linazidi kukua. Ifike mahala traffic offences iwe ni two way approved. Yani unaniandikia kosa na mimi kukubali kosa aidha nasaini au naingiza namba ya siri kukubali kosa. Hii mambo ya askari kukaa baa na kuingiza namba za magari waliyokamata mchana ili kufikisha target inaumiza sana tu.
 
Umenikumbusha mkuu, Mimi nilisimamishwa na trafiki January mwaka huu, baada ya ukaguzi sikupatikana na kosa, akacheki kama ninadaiwa, ikaonekana niliandikiwa mwezi wa 11 mwaka jana na sijawahi kulipa pia deni limefika 60000. iliniuma sana sababu kwa akili zangu sina kumbukumbu ya kuandikiwa kosa mwezi tajwa. Nikakomaa kwanini sikupewa risiti nilipoandikiwa nilipata Maelezo ya kiboya sana hata nilipokwenda kwa mkuu wao sikupata msaada wowote.
 
Pole! Naona wamegeuzwa kuwa chanzo cha kukusanya mapato.
 
Hakuna cha mkuu wla nn mtasumbuk bure wote lao moja cna hamu na hawa viumbe.nchi hii ingekuw daladala ningeshashuka nakusameh naul kbs
 
Hawa jamaa ni hovyo kabisanahisi wapo kwaajiri yakukusanya kodi
 
Hawa jamaa ni hovyo kabisanahisi wapo kwaajiri yakukusanya kodi
Pamoja na kukusanya hiyo kodi waliyotumwa hakuna haja ya kumuonea mtu kwa kumbambikizia kosa jingine.
 
Hawa jamaa wamegeuka kero nakutugeuza madereva kua miradi yao na kwahili wamefanikiwa kwelikweli maana wanajenga mahekalu na kununua mikoko kwa pesa zetu wanazo tunyang’anya kwa nguvu mabarabarani
 
Ndio maana mijeda huwa inawatwanga hawa jamaa,, na hiyo 30 waliozidisha mkuu hukujuwa kosa lako, pengine yale matamshi mlikuwa mnafokeana washkaji wakaongeza. Pole sana kiongozi! Inasikitisha kwakweli.

Inshort polisi wana pesa za kumwaga na zote zimetokana na njia zisizo za halali.
 
Hawa jamaa wamegeuka kero nakutugeuza madereva kua miradi yao na kwahili wamefanikiwa kwelikweli maana wanajenga mahekalu na kununua mikoko kwa pesa zetu wanazo tunyang’anya kwa nguvu mabarabarani

Fact...lakini pesa za hivyo huwa hazimuachi mtu salama.
 
Hawa jamaa ni hovyo kabisanahisi wapo kwaajiri yakukusanya kodi

Polisi inakusanya pesa sio mchezo baba.hata kama gari lako ni full insurance ila watatafuta kisababu mara sijui stika mara oh fire extinguisher imechekaa tunataka mpya sijui tairi upande mmoja imelika...
 
Kuna wengine nilikutanao Nyamikoma nafikiri ni mkoa mpya Simiyu wakaniandikia faini eti sikusimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu na kuwasha taa za hazard,nilipotaka wanifafanulie vizuri sheria hiyo wakanionesha msg zao za magroup eti lazima nisimame niwashe hazard ndio nivuke na wakati sheria haiko hivyo.Basi nililipa faini nikaendelea na safari yangu,ushauri kwa jeshi la polisi mambo mengine yalitungwa na mkoloni ili atawale zvr fanyeni marekebisho ya sheria na waelimisheni askari wengine hawajui kabisa!
 
Tatizo ukiwa mwananchi wa kawaida ukahoji haki yako unaitwa mjuaji na ndio mwanzo wa kuongezewa makosa hapo.
 
Back
Top Bottom