Trafiki Dar kufumuliwa na Sirro

Trafiki Dar kufumuliwa na Sirro

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,536
Reaction score
27,447
Katika hali ya kutojitambua na kwa Maksudi kumsusia IGP SIMON SITRO , KANGI LUGOLA "SHAOLIN" na HON J POMBE MAGUFULI " , ili tu aonekane mradi wa Mwendokasi ameushindwa, Kikosi cha Polisi wa Usalama Barabarani wamekuwa mstari wa MBELE KUSUSIA/ kuacha kwa maksudi wanao hujumu DAR/MWENDOKASI na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha.

Baada ya mwendokasi kujengwa, baadhi ya daldala ziliondolewa ikiwa pamoja na Mbezi-Posta- ,Mbezi-KAriakoo,na nyongine nyingi ili watu wapande mwendikasi of which kule analipa kodi na nchi inajiendesha.



NINI KIMETOEA

HUJUMA YA KWANZA
mwendo 4.jpeg
mwendokasi 1.jpeg
mwendokasi 2.jpeg
mwendokasi 5.jpeg
mwendo 4.jpeg
5.jpeg

HIVI KARIBUNU , daladala za Makumbusho -Posta na Makumbusho _Kariakoo kupitia Sinzan na Sheiklango zenye msitari mwekundu zimeshiriki kwa wazi kumhujumu eais mpendwa Magufuli kwa usaidizi wa maafisa usalama barabarani.

Daldala hizo,kila ifikapo saaa kumi jioni, zinabadili njia, mfano ukiwa Posta wanasema wanaishia Magomeni, watu wanapanda mpaka magomeni , wakifika kituo cha "fire" wanasema inaishia manzese , wakifika manzese wanasema inaishia Sinza , wakifinga shekilango wanasema bamaga na wakifika Bamaga, wanageuza pale ustawi wa jamii na kurudi njia nyingine.

HUJUMA YA PILI.
WALE WA KARIAKOO MAKUMBUSHO, wao ikifika saa tisa alasiri husema wanakwenda MABIBO, NI SEHEMU FUPI NA HAKUNA FOLENI, kwahiyo wanajinufaisha huku wakijua hawana TLB ya kwenda MABIBO, kinachotokea ni wale wenye ruyti ya MABIBO kujiona hawana lao na kuichukia serikali, wakishtaki kwa Mrindoko, AKIBOA naye hacchukui hatua.

kumbuka daldala nyingi mjini, kama ilivyo bodaboda za "Posta" zinamilikiwa na polisi na ndio maana mchana kweupe wanabadili njia/route.

HUJUMA YA TATU
Mwendokasi kwakuwa zimekuwa chache, na nauli ni mia sita hamsini 650 kwa kituo, basi watu wa daladala wanaleta KARIAKOO -MBEZI KWA TSHS 1000 na yanajaa, huku mwendokasi ukila mafuta bila abiria, hii ni uhujumu uchumi kabisa.

HUJUMA YA NNE
Magari ya Seriakli, hasa STL,PT, AG, J ,JK, CS, na wengine wenye namba binafsi wame endelea kutumia hii barabara ya mwendokasi as if they are sacred nd special, mbaya zaidi MAJAJI WA MAHAKAMA KUU NA MAHAKAMA YA RUFAA , ambao ndio walinda sheria wanapita, jana tarehe 1-10-2019 polisi walikamata magari kama 40 tu, na kwa aibu hata ITV walipotangaza kukamatwa kwa hayo magari hawakudhubutu kuonyesha picha, maana ni aibu, kila mtu kawa kambale wakati serikali tena MAGU alisema gari ikipita huko ingolewe matairi.


NINI CHA KUFANYA?

1. IGP SIMON SIRRO, wewe ni mweledi na mchapa kazi wetu, fumua kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar, waliopo wapeleke huko katavi na mlele au lake tanganyika wakakae huko.

2. MAKONDA tunakuamini sana, hii issue kwako ni sekunde tu, ingia barabarani mwenyewe , kamata magari , uliza abira watakutonya na ufuatilie wamiliki, nakwambia utalia maana yote ni ya vijana wako .

3. MKURUGENZI LAART/SUMATRA ingia barabara kwa kushtukiza, tena hata kama mtajilipa overtime we dont care, kaeni usiku mtakamata magari yote, wekeni vijana wenu vituoni, wapande kwenye hizo daladala na wawarekodi hao madereva.

4. waziri wa ujenzi na uchukuzi, kama hawa wote hawachukui hatua , na mh Pombe magufuli hajui hili, basi chukua hatua, haikugharimu, kumbuka rc wa Moro alilala lala akaliwa kichwa, ingia barabarani hata leo, utalipwa, maana rais huwa ana appriciate kazi nzuri za mawaairi wake.



5.magari binafis, tena mbele ya kituo kikuu cha POLISI DAR, kinaitwa "stesheni" kwa sisi wakazi wa mbagala imekuwa rasmi, hawa gari ndogo hawana leseni za kubeba abiria lakini wanabeba, yena na baadhi ya polisi traffick ni abiria na wanaona sawa tu, nasema RAISI MAGUFULI ANAKWAMISHWA NA SISI, ANA NIA NJEMA , WATENDAJI WANAMUANGUSHA.
Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka maarufu kama mabasi ya Mwendokasi umekuwa tegemeo kuu kwa wasafiri Dar es Salaam lakini huduma hiyo imekumbwa na vurugu.




HIVI NDIVYO WENGINE WALIVYORIPOTI.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema Jeshi la polisi kwa kipindi cha kuanzia Septemba 19, 2019 hadi sasa linashikilia jumla ya magari 50 huku 19 yakiwa ya Serikali na 31 binafsi kwa kosa la kupita katika barabara ya mabasi ya mwendokasi.

Akizungumza leo Oktoba 1, 2019 Kamanda Mambosasa amesema kuwa japo kuna watu wamezoea kutoa faini pindi wanapokiuka sheria, lakini kwa upande wa barabara ya mwendokasi hakutakuwa na utaratibu wa kutoza faini badala yake watu watapelekwa rumande.

''Unakuta mtu anandaa fedha kwanza afu anaingia mwendokasi kwakuwa faini ni elfu 30, katika mwendokasi sitakubali kutoza faini, hatuko kwa ajili ya kutafuta fedha tunachotaka nikuleta nidhamu ya matumizi sahihi ya barabara hiyo, atakamatwa mhusikia atapelekwa polisi, atawekwa rumande maandalizi yatafanyika kupelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali na kufunguliwa mashtaka'' amesema SACP Mambosasa.

Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa magari pekee yanayoruhusiwa kutumia njia hizo ni yale yanayowahisha wagonjwa hospitali na kwamba ikitokea gari la wagonjwa limetumia njia hiyo likiwa halina mgonjwa lazima litakamatwa.





WEBSITE YA SU ATRA/LART INA MAAFISA HAWA, walipaswa woteke ofisini waingie mtaani na kujua yanayoendelea


Full Name
Tel No​
Gilliard W. Ngewe
Director General
255 222 197 501​
Tumaini Silaa
Director, Legal Services
255 222 197 506​
Samwel D. Keenja
Ag. Director, Finance, HR & Administration
255 222 197 551​
Ahadi Chacha
Director, Performance Audit
255 222 197 508​
Makiri Ngangaji
Ag. Director, Economic Regulation
255 222 197 519​
Johansen J. Kahatano
Director, Road Transport Regulation
255 222 197 531​
Eng. Lameck E. Kamando
Ag.Director, Railway Regulation
255 222 197 529​
Dolores M. Ng'wandu
Manager, Tariffs & Competition
255 222 197 535​
Jumanne A. Swavila
Manager, Procurement & Supplies
255 222 197 512​
Godfrey U. Nsato
Ag. Manager, Corporate Communication
255 222 197 521​
Godfrey U. Nsato
Manager, ICT
255 222 197 533​
Ahmad Mwenyemanga
Manager Performance Audit
255 222 197 530​
Neema M. Mhagama
Manager Human Resource & Administration
255 222 197 504​
Samwel D. Keenja
Manager, Finance
255 222 197 551​
Leticia Mutaki
Ag. Manager, Legal Affairs
255 222 197 573​
Leo Ngowi
Manager, Road Licensing and Monitoring
255 222 197 531​
Makiri Ngangaji
Manager, Planning, Research & Development
255 222 197 519​
Geoffrey L. Silanda
Manager, Road Technical, Safety & Environmental Regulation
255 222 197 531​
Fahamuel E. Mnkeni
Manager, Regions Operations
255 222 197 575​
 
Am sorry; but you are a nincompoop. Yaani unataka abiria wanaokwenda au kutoka Kijichi wasipate usafiri wenye staha (wanaoupata kwenye magari ya watu binafsi)? Hivi nyie watu mna matatizo gani? Yaani mnafurahia matatizo ya wenzenu sio?
 
Kila nkijitahidi kusoma sion mantiki na ushikaman wa habari. Kumbe utungaji ni mgumu hivi ?
 
Am sorry; but you are a nincompoop. Yaani unataka abiria wanaokwenda au kutoka Kijichi wasipate usafiri wenye staha (wanaoupata kwenye magari ya watu binafsi)? Hivi nyie watu mna matatizo gani? Yaani mnafurahia matatizo ya wenzenu sio?
hawa binafsi hawana leseni za kutubeba, ikitpkea ajali huwezi fidiwa kama abiria, pia majambazi wanapora na kuteka kwa kujifanya wanabeba abiria.
matukio ya wanawake kubakwa nako ni mengi tu, kwa hixi gari za kuchangia.
 
hawa binafsi hawana leseni za kutubeba, ikitpkea ajali huwezi fidiwa kama abiria, pia majambazi wanapora na kuteka kwa kujifanya wanabeba abiria.
matukio ya wanawake kubakwa nako ni mengi tu, kwa hixi gari za kuchangia.

Unalazimishwa kupanda? Acha wanaohitaji wapande.
 
Unalazimishwa kupanda? Acha wanaohitaji wapande.
Wapande wakiwa salama, wakiumia kodi yangu inawatibu.

ajali ya moto morogoro kodi zetu zimewatibu wale watu, tena kukodiwa ndege, ni mabilioni ya fedha yametumika.
Tunasisitiza, kuanzia kesho hayo magari SUMATRA watayakamata, jioni pale stesheni , mbagala watakuwa maji matitu, chamazi, kwa mbiku na kibondemaji.
 
Mwandishi unastahili ukawahi nsfasi Milembe, unachosha watu
 
Hata polisi haswa traffic wamekuwa wanyanyasaji wa raia na ni kama hakuna sheria. Wanakuweka ndani wanavyotaka na lazima utoe pesa. Utalalamika wapi na ni mfano kutoka juu?
 
Suala la hawa ma traffics ni nchi nzima! Nchi imekuwa lawlessness
 
Hata polisi haswa traffic wamekuwa wanyanyasaji wa raia na ni kama hakuna sheria. Wanakuweka ndani wanavyotaka na lazima utoe pesa. Utalalamika wapi na ni mfano kutoka juu?
Serikali yetu kila ikiweka Sheria Kali vp.ndio kwanza wanamtengenezea Karan na hakimu ulaji wa rushwa.wao ndio wamuzi wa mwisho
 
Hoja ya msingi unayo ila namna ulivyoandika ni kama umepiga miluzi mingi sana na mbwa amepoteza mwelekeo hajui aanzie wapi kuwinda
 
Kuhusu usafiri, huwezi ukamsubirisha abiria akae muda mrefu kusubiria mwendokasi hususani ile mida mibovu, huku kuna daladala zinaelekea njia moja hiyohiyo...muda mwingi mwendokasi hazijipangi kisawasawa kupunguza abiria stendi.
 
Back
Top Bottom