Uko wapi?
Hapa niko jirani na kituo cha trafic naendelea na shughuli zangu na trafic kama kawaida wanaendelea na kazi yao ya kukusanya hongo. Kila gari linalopita linasimama konda au tingo anatoa kitu kidogo safari inaendelea, magari mengine ni mabovu hata kwa kuyaangalia tu lakini wakishatoa wanaruhusiwa tu. Kwa mtindo huu ajari zitakwisha ? Sijui nichukue video yao kama J. Muro ingawa haisaidii kitu maana inaonekana hata wakubwa hapa wana mgao wao, kuwa wazalendo jamani.
Rushwa kuiondoa siyo jitihada za traffic. Umejiuliza kwa nini mtu anatoka na kushawishi kutoa RUSHWA? kuna tatizo katika mifumo yetu. Kama sumatra wamemupa route, kama TRA wamemupa lesseni ya biashara na gari lake bovu, unadhani polisi ataanzia wapi kukomesha hali hiyo? hizi taasisi zote, ni wehu tu, masaburi @ work every nukta, usitegemee ajali kuisha.
kuna OCD mmoja alisimamia sheria ya kupiga disco kusini mwa tanzania. aliyekuwa anapiga disco, alikuwa ni KOMBA. Mda ulipofika OCD akaeenda kumkumbusha mwisho wa makubaliano yetu 6 usiku, watu wakasema tunataka hadi majogoo, komba akamsihi amruhusu, OCD akagoma, komba akamwambia ukininyima ruhusa ya kukesha, iko sehemu nitaruhusiwa. Komba akapiga simu, akaruhusiwa na yule OCD kuamriwa kumlinda komba mpaka majogoo. Kulipokucha, OCD alifatwa na RPC wake kuwa anaitwa kwa mkuu wa mkoa, alipigwa transfer na kushushwa cheo hadi mshauri wa mgambo wilaya.
walioshikilia system wakiwa waovu, hata wanaoisaidia sysytem kuendelea kuwepo watakuwa waovu, hautapata msafi hata siku moja
Yupo barabarani..., Ukweli tutawalaumu bure kwani hali ya maisha ni mbaya kwa kila mtanzania na tumeoza kuanzia kichwa hadi vidoleni, hiyo rushwa ndugu yangu huenda kugawanwa na wakubwa zao na wasipofanya hivyo wako hatarini kupelekwa Mtimbira, kawaulize pale Chalinze walivyokosea tu wote wakapigwa PI ktk barabara maarufu
Kwa kweli habari ndiyo hiyo. Mkuu wa kaya ndiyo bosi wa mabosi wanaosimamia hongo hizo. Hao wadogo wanapochukua hongo hupeleka mgawo kwa walioko juu. Angalia ngazi yao ya madaraka na vivyo hivyo hongo hizo huwafikia huko huko. Hii ni Tanzania na lazima ulielewe hilo. Vinginevyo kama una uchungu na nchi hii basi tukiitisha maandamano ya kuwaondoa madarakani hao wanaosimamia hongo/rushwa basi ujitokeze.
Uko wapi?
Cha ajabu wakiona DFP, ST, au gari ya mwarabu wanaangalia pembeni, kama hii kusanya kusanya ingekuwa haiendi hadi kwa wakubwa hawa wadogo wangekuwa wanakamatwa kirahisi muno, we kamanda wa Iringa hebu jaribu kushtukiza sasa hivi halafu wakague hao walioko barabara zinazoingia Iringa mjini uone kila mmoja ana shs ngani na kazipata wapi, saa hizi.
Ukitaka utamu wa Askari hawa na wasikupe shida toka Bukoba hadi Songea wee tafuta na nunua pesa bandia za Tsh 10,000/=, kila wakikusimamisha toa aione kidogo halafu ikunjekunje kwa sanaaaa halafu naye ataipokea haraka haraka na kuificha tena walivyo huwa hawapendi wenzie wajue kuwa hapo imetoka u..ten ili baadaye awazime, jioni wee umeshafika safari yako yeye anafunga mahesabu au anaagiza bia basi hapo ndio msala unakuwa wake
hatari hatari zaidi ya umemeRushwa kuiondoa siyo jitihada za traffic. Umejiuliza kwa nini mtu anatoka na kushawishi kutoa RUSHWA? kuna tatizo katika mifumo yetu. Kama sumatra wamemupa route, kama TRA wamemupa lesseni ya biashara na gari lake bovu, unadhani polisi ataanzia wapi kukomesha hali hiyo? hizi taasisi zote, ni wehu tu, masaburi @ work every nukta, usitegemee ajali kuisha.