Heshima kwenu wakuu,
Kwanza nalipa pongezi jeshi la Polisi kwa kazi kubwa ambayo wanafanya haswa kitengo cha usalama barabarani kwa kazi kubwa mnayofanya.
Pili ningependa kutoa ushauri kwa traffic mnaoongoza magari hapo moroco acheni hii tabia ambayo imeanza kuota mizizi, hivi mnawezaje kuruhusu magari ya upande mmoja nusu saa mzima na hakuna msafara wowote wa kiongozi unaopita?
Leo asubuhi mmetukalisha dakika 33 tunaotoka magomeni kwenda kawe na jioni pia mmefanya hivyo hivyo.
Afu hii tabia ya kukamata watu wanaowaambia ukweli imeanza lini?
Masikini mzee wa watu mmekalisha kwenye foleni almost 40 minutes, anakuja kuwaambia upupu mnaofanya sio fair mnamweka ndani.
Naomba kama mmeshindwa kuongoza magari basi acheni taa zifanye kazi yake na nyie mbaki hivyo hivyo kama mlivyojigeuza TRA.