Traffic - huu ndio utaratibu au magumashi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Traffic - huu ndio utaratibu au magumashi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kizamani, Jun 25, 2012.

 1. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari za jioni wana JF wenzangu na wapenda maendeleo wote kwa ujumla.

  Ijumaa jioni, nikiwahi mjadala wa kufunga bajeti nilikamatwa kwa traffic. Nikiwa katika hali ya kuwahi kuangalia bajeti nikitokea Mwenge kuja ubungo, nilipita kwenye service road inayotokea sisimizi ambapo traffic waliokuwa wamejibanza walinikama. Nilikuwa sina jinsi ila kuwa chanzo cha mapato ya taifa letu, walifanya kazi yao.

  Niliandikiwa buku 30 kwenye fomu ya "notification of traffic offences" na kwa sababu sikuwa na kiasi cha kutosha ilibidi nitafute Mpesa karibu, kilichonishngaza wakati wa kulipa niliona ile pesa inasokoteshwa kwenye origina ya ile fomu na mimi kupewa kopy yake. Ilibid nidai risiti ya serikali ambapo niliambiwa inabidi nisubiri yule traffic, ambaye nilisoma jina lake "Mwamakule", amalize kazi ndipo tuongozane mpaka ostabay polisi ndipo niandikiwe, nikala na matisho mengine mengine kwamba nikifika naweza kuwekwa ndani na mambo mengine aliyoongea, nikaona isiwe so, nikala kona.

  Ishu yangu:
  Je hii fomu ya traffic offences ni sawa na risiti halali ya serikali. Inafanyiwa oditing? je ni haki yangu kupewa risiti pale au kuzungushwa. Ni lazima kuwa makini kwani unaweza kuta buku 30 yangu either ilinywewa laga au kusuuzia rungu. Naomba mnielimishe nyie wenye experince na haya mambo ya traffic, sio kwamba nawalaumu kwa kufanya kazi yao.

  Mwito wangu kwa wapenda maendeleo:
  1. Ujue haki yako. Sio tu uende kwa mjumbe uambiwe leta buku kumi ili uandikiwe barua na wewe utoe tu, jua bia ya srikali ni shilingi ngapi.
  2. Mnaonaje wana CDM wenzangu kwamba tutakavochukua nchi 2015 tuwashauri traffic na watumishi wengine wa serikali kwamba kama anaenda sehemu ambayo anajua atapokea malipo kwa naiaba ya serikali ni vema akwa na kitabu cha risiti halali ya serikali. Hii itasaidia kuondoa mianya ya kupoteza mapato ya serikali.
  3. Nakushauri wewe unayesoma hii thread ingia CDM kwani utajifunza mengi. Mimi ni kama mwezi tu nimejiunga CDM na kuweza kuhudhuria vikao na wanachama wengine na nikajifunza mengi sana.
   
 2. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ushaliwa weye
   
 3. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  notification of traffic offences ni taarifa ya traffic police ya kuelezea dereva ana kosa fulani na sio risiti na haifanyiwi auditing.
  pesa alikwenda kuitumia.
   
 4. B

  Bob G JF Bronze Member

  #4
  Jun 25, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwanini na wewe ulitanua? mtu makini anaheshimu sheria na taratibu za nchi, hakuna sababu inayoweza kuhalalisha uvunjaji wa sheria na walikulipisha kiasi kidogo adhabu kwa kosa hilo kwanza una kula wiki segerea then fain 250,000/ ukitanua unachelewa zaidi ukikamwa kuliko ungefata sheria, Na foleni mara nyingi zinaletwa na watu kama nyie mnaodhani ninyi ndo mnaharaka kuliko wengine na ndo Ubinafsi unapo anzia hapo
   
 5. GP

  GP JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mi niliwai kupita ile ya upande wa pili kuingilia mawasiliano kutokea pale kona ya chuo, askari wakanikamata, wakakuta gari ina makosa mengine, nikapelekwa ubungo ndani polisi wakataka 40K, nikawaambia sina nna 20K wakakomaa kinoma na vitisho vingi!,
  nikawaambia natoa 40K ila nataka risiti ya serikali ile ya njano wakaniambia niende magomeni watanipa risiti huko, yani longolongo jingi, but nilienda magomeni nikalipa na wakanipa risiti, nikarudi ubungo kuchukua ndinga, jamaa kuwaonyesha risiti walinimaindi kimtindo nimewanyima hela ya dezo!.
  actually niliamua kwenda kulipia magomeni kwakua bado nilikua na mizunguko so ile faini ilikua inaniwezesha kupiga misele kwa wiki nzima bila kukamatwa tena.
  TRAFIKI BONGO NJAA TUPU.
   
 6. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  pia sijui kwanini traffic akikusimamisha lazima akuulize kazi yako?
   
 7. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Namimi nikiwa traffic oysterbay niliona wanaokatiwa kwenye hicho kitabu wanapewa copy waendekulipia juu ili wapewe risti kama ameandika inamaana ataenda kulipia mwenyewe oysterbay sema risti ndo atabaki nayo!!
   
 8. GP

  GP JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  HAKUNA KITU KAMA HICHO MKUU!,
  hizo hela wananywea BIYA, kwanza inasemekana wana vitabu feki, kwahiyo kua makini.
  wewe just imagine kakukamata ubungo alafu anakwambia uende ostabei na wewe ulikua unatanua uwai kimara stop ova kwa mtitu kula mbuzi choma na mpwa Fidel80, unapiga mahesabu kwenda ostabei kweli?, wanakwambia vile ili uone ni usumbufu then uwape tu hela wakuandikie notification feki.
  mi nilikomaa nao nikapewa risiti yangu!.
   
 9. Kizamani

  Kizamani JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [​IMG] JF Bronze Member [​IMG] Array

  Join Date : 5th October 2011
  Location : UK Manyasi
  Posts : 702
  Rep Power : 478
  Likes Received99
  Likes Given36

  [h=2][​IMG] Re: Traffic - huu ndio utaratibu au magumashi[/h]
  Kwanini na wewe ulitanua? mtu makini anaheshimu sheria na taratibu za nchi, hakuna sababu inayoweza kuhalalisha uvunjaji wa sheria na walikulipisha kiasi kidogo adhabu kwa kosa hilo kwanza una kula wiki segerea then fain 250,000/ ukitanua unachelewa zaidi ukikamwa kuliko ungefata sheria, Na foleni mara nyingi zinaletwa na watu kama nyie mnaodhani ninyi ndo mnaharaka kuliko wengine na ndo Ubinafsi unapo anzia hapo

  Bob G, ishu hapa si kukamatwa na kutanua, ishu hapa ni kulipa hela kwa traffic na kupewa risiti halali ya serikali ili kulinda mapato. Unavosema kupigwa segerea na mambo mengine huna tofauti na yule traffic Mwamakula. No any logic hapa unapodai risiti ya serikali unaaambiwa utapelekwa mahabusu. I dont think it is right. Hatutaki ujanjaujanja sasa hivi. ​
   
Loading...