Kuna askari wa usalama barabarani wanasimama karibu na stand ya Sanawari wakikagua magari yanayoelekea Ngulelo. Askari hawa wanafanya dhuluma kubwa ya kubambikizia watu kosa la kupita na taa nyekundu kwa wanaotokea upande wa Mount Meru Hospital. Kama sio dhuluma basi mfumo wa hizo taa uangaliwe. Leo nimepita na taa za kijani zikiwaka, cha ajabu askari mmoja aitwaye Hamisi akang'ang'ania kuwa nimepita na taa nyekundu. Wanachofanya ni kumwambia mwenzake kuwa "si nilikuambia akija hapa atabisha, mwenzake anajibu ni kweli". Tabia hii nimeisikia kwa madereva wengi. Tunaomba kikosi cha usalama barabarani hapa Arusha kiangalie hili madereva watozwe faini kwa makosa ya kweli. Elfu thelathini ya kusingiziwa imeniuma sana.