tradecarview.com ni wakweli?

Katabazi

JF-Expert Member
Feb 18, 2007
353
19
Salaam wana JF!
Naomba kujua kama kuna mtu aliyewahi kununua na kupata gari kutoka kampuni zilizomo kwenye site hiyo hapo juu?au kama kuna aliyewahi kupata matatizo nayo. Maana bei wanazotoza naona ni za chini sana kulinganisha na makampuni mengi niliyowahi kuyasikia.Naomba ushauri.
 
Uwe makini kuna wengine wanamagari yao dar es salaam ila wanajifanya yako japan au popote duniani kwahiyo ukiagiza utapewa tu halafu baada ya siku kadhaa unaweza kushangaa umeibiwa gari hiyo au umekamatwa nayo ya wizi

uwe makini sana ndugu
 
Kuwa makini mkuu,hiyo site ya Tradecarview.com ni site ya wadau mbali mbali wanouza magari.
Hakuna kampuni inyoitwa Tradecar view na pale ni kama ubao wa matangazo tu.
hat hivyo kuna kampuni za kitapeli pale na kampuni zinazofanya biashar nzuri ti.Mimi nimefaidika na kampuni moja kati ya zilizomo humo.
 
Mkuu ukihitaji Kampuni zenye Uhakika katika web site ya Tradecarview unaweza kuni PM kama ninayo nafasi nikakupa info. Kampuni zilizo nyingi ktk hii web site ni za Warushia , Waarabu ,Waingereza ,Wamarekani na Wanigeria ,Waindonesia na Wathailand .. Usipo kuwa makini utapigwa vizuri sana. Hata Wajapan siku izi wamekuwa wajanja sana.
 
Ndiyo, tradecarview.com ni wa kweli.

Unachotakiwa kujua ni kwamba, wao si wauzaji wa magari, tradecarview ni kama watangazaji tu, wao wanatoa huduma ya kutangaza magari yanayouzwa na wauzaji wa magari. Ni watu wengi tu wanaonunua magari hapo (mara nyingi mnadani unapata kitu kwa bei rahisi kidogo!).

Kama walivyosema wadau hapo juu, unaweza kupata gari bei chini lakini kuwa mwangalifu sana! fuatilia reputation ya hiyo kampuni, imekuwwepo tradecarview kwa muda gani, hawa tradecarview mara nyingi ni waangalifu wakipata malalamiko kuhusu kampuni wanaifungia kutangaza, mpaka mwizi huyo ajipange upya aingie na jina lingine.

Pia jitahidi kufuatilia details zote za gari, mara nyingi wezi hawa wanakuwa na picha tu za hayo magari, ukimuomba details kama deragistration au picha zaidi na service record anakuwa hana, usijiridhishe mapema, ulizia hata kwa watu wengine kama walishaagiza na hiyo kampuni, kampuni zingine ni za ukweli lakini wanaweza kukutumia gari ambayo hukuichagua, au MBOVU!!!!

YOTE KATI YA YOTE, UKITAKA KITU NAFUU UKUBALI KUTAKE RISK.
 
kweli kabisa hawa jamaa unakuta wanastock kubwa sana ila ninachoona kila mtu anatupia mzigo wake pale kuuza na wengine na hivyo makanyaboya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom