TRA yaweka rekodi ya karne, yakusanya Trilioni tatu kwa mwezi Desemba Pekee

Hata wakusanye 50B hazina maana yoyote kwa common mwananchi kama huduma muhimu hakuna mtaani.

Watu wanahitaji umeme wa uhakika,maji etc

Kujifaragua makusanyo wakati umeme wa mgao kisa mitambo mibovu ni sifa za kijinga.
 
Huduma zipi ambazo hazipo? Aliyekwambia kama Mkoa wako hakuna umeme ni Mikoa yote ni nani?
 
Hata wakusanye 50B hazina maana yoyote kwa common mwananchi kama huduma muhimu hakuna mtaani.

Watu wanahitaji umeme wa uhakika,maji etc

Kujifaragua makusanyo wakati umeme wa mgao kisa mitambo mibovu ni sifa za kijinga.
Kaaa kwa kutulia wewe. Kwani wewe huoni namna serikali ilivyoleta mapinduzi makubwa katika huduma za kijamii kwa kuzisogeza karibu kabisa ya mwananchi?
 
Nilikuwa naangalia nani kaandika hiyo habari baada ya kumfahamu kutoka TRA nikachoka sana. Huu mwaka wa uchaguzi CCM inatumia kila aina ya ulaghali kutapeli kura.
 
Hata kama hizi ni data za ukweli..., kuna installment ngapi kwa mwaka na installment ya kwanza na pili walikusanya ngapi ? Au ni sababu watu walikuwa hawajalipa huko nyuma ndio wamekuja kulipa kwa haraka na kuogopa penalty ?

Kama December wamekusanya hizo na miezi iliyopita walikuwa wanakusanya ndogo huoni kwamba huko nyuma kulikuwa na walakini ?

Jaribu kuangalia mambo kwa critical eye...
 
Ukitaka ukione cha mtema kuna na kujuta kazaliwa basi wewe Gusa pesa alizotoa Rais Samia kwenda kufanya shughuli za maendeleo na kuwapatia huduma Wananchi.

Zinaguswa sana, mpaka CAG anaona kuna upotevu, ni ahatua gani zinachukuliwa? Au zimechukuliwa kuwawajibisha walitafuna pesa kwenye report ya CAG? Hakuna
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari ikufikie popote pale ulipo kuwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imetangaza kupitia menejimenti yake kuwa imefanikiwa kuweka rekodi ya kipekee kabisa tangia kuanzishwa kwa mamlaka hiyo kwa kuweza kukusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi Trilioni tatu na point.

Haijawahi kutokea katika Historia ya Taifa letu .imetokea wakati huu kutokana na mazingira mazuri ya kisera na kisheria yaliyowekwa na serikali ya Rais samia yaliyochochea ongezeko la biashara nyingi zilizo pelekea kuongezeka kwa wigo wa kodi.

Ndugu zangu ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa watu wapo huru na wanajisikia fahari kufanya na kufungua biashara nchini,watu wapo huru na wanajisikia fahari kulipa kodi.hii ni baada ya maafisa wa TRA kujenga mahusiano mazuri na wafanyabishara kama ilivyoagizwa na mheshimiwa Rais wetu mpendwa Mama Samia aliyekataa Kodi za dhuluma na machozi..

Kwa sasa wafanyabishara wanawaona maafisa wa TRA kama watumishi wao na siyo maadui zao na kuishi kwa kuviziana na kukimbiana na kukimbizana Mitaani.lakini pia TRA kupitia kitengo chake cha elimu kwa mlipa kodi imeongeza sana elimu kwa watu na hivyo kuwajengea uelewa juu ya masuala ya kodi na kikodi. Hivyo watu hasa wafanyabiashara kuelewa nini kinapaswa kulipwa na wafanye nini wanapoona hawajaridhika na ukadiliaji wa mapato.

Lakini pia kumekuwa na muamko kwa wananchi katika kudai risiti baada ya kufanya manunuzi ya bidhaa, kwa kutambua kuwa ni kupitia njia hiyo ndio fedha zao zitarejea tena kwao kwa njia ya kujengewa zahanati,vituo vya afya,shule,madarasa, barabara, usambazaji wa maji safi na salama,huduma za umeme,elimu bure,Ruzuku za mbolea,kununua vifaa tiba,madawa na kuajiri watumishi wa afya mahospitalini pamoja na walimu shuleni.n.k.

Hongera sana TRA kwa weledi wenu mkubwa na uaminifu wenu kwa kuhakikisha kila senti inaingia na kwenda hazina ili nchi iweze kufanya maendeleo kwa kujenga miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi.

Hongera sana Rais Samia na Serikali yako kwa kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara mpaka sasa wanafanya biashara kwa uhuru na amani. Kikubwa serikali iendelee kudhibiti mianya yote itakayoonekana kuvujisha na kupoteza mapato halali ya serikali.Elimu kwa mlipa kodi na wananchi iendelee kutolewa na liwe ni zoezi endelevu ili ifike hatua somo hilo liwe kichwani na katika mioyo ya watanzania ili kila mmoja ajione fahari kulipa kodi.

Lakini pia kodi hizi zitumike vizuri pale zinapopangiwa matumizi na siyo watu wanatokwa jasho kulipa kodi na kukusanya kodi halafu linatokea jitu linafanya ufisadi wa mabilioni kwenye miradi ya serikali au kwa kufanya ujanja ujanja halafu linaendelea kutamba mitaani kama jogoo bila kuchukuliwa hatua zozote.hii ikifanyika na kuachwa itawakatisha tamaa walipa kodi wazalendo na wakusanya kodi wazalendo kwa kuona kuwa jasho lao linapotea bure tu.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
"Lucas Hebel mwashambwa", sasa jina lako limetimia na unagaa ka uteuzi.
 
Kama ni ulaghai basi nawewe lete takwimu zako hapa.
Mimi ni kada mwenzio tena kiongozi ngazi ya wilaya. Lakini sijidhslilishi kwa kiwango chako. Bahati nzuri nimewahi kupitia vetting Yako ofisini Kwa Peter Magoti imeandikwa, "NONE TO DELIVER" kwamba hufai kuongoza. Unajipendekeza mno hutoweza kuwaheshimu raia zaidi ya mteuzi. Hizo takwimu zimepikwa na Kayombo na Deus kwa makusudi ya kuzima kileeeee unachokijua. Ungeacha wengine waongee sio wewe tunakucheka hapa Lumumba kwa Mrisho muuza vitenge. Kuwa smart bro.
 
Kwahiyo umeme utaacha kukatika

Back
Top Bottom