Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Chama cha wafanyabiashara Mkoa wa Arusha (TCCIA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA )wameanza kuwanoa wafanyabiashara mkoa wa Arusha ili watambue umuhimu wa kulipa kodi ya majengo na mabango kwa mujibu wa sheria baada ya kuhamishiwa TRA.
Semina hiyo inayoendeshwa na Afisa elimu wa walipakodi (TRA )kanda ya Kaskazini, Eugenia Mkumbo, aliwataka wafanyabiashara hao kuzingatia matakwa ya serikali katika kuona umuhimu wa kulipia kodi ya mabango .
"Awali mabango yote yalikuwa yakilipiwa katika halmashauri lakini utaratibu Huo umebadilika kwani kila Mfanyabiashara kwa sasa mwenye bango atapaswa kulipa kodi TRA jambo litakalosaidia kupunguza utitiri wa mabango yanayoweza kugeuka uchafu" Alisema Mkumbo
Ameongeza kuwa manispaa itaendelea kutoa vibali Vya mabango kwa wafanyabiashara watakao kuwa wakiomba kutaka kuweka mabango kulingana na sheria inavyoelekeza.