TRA yaufunga mgodi wa Almasi wa Elly Hilali Shinyanga

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani Shinyanga imeufunga mgodi wa uchimbaji wa almasi wa Elly Hilali ulioko Mwadui Shinyanga kwa muda usiojulikana kwa kosa la kushindwa kulipa deni la mapato ya serikali zaidi ya shilingi milioni mia tatu sabini na nne na laki tisa na sabini huku wafanyakazi wa mgodi huo wakilalamika kuathiriwa na kitendo hicho.

Akizungumza na ITV kuhusu sakata la kufunga mgodi huo wakala wa ukusanyaji mapato wa TRA Bw.Lyasuka Ibrahim amedai TRA imelazimika kuufunga mgodi wa almasi wa Elly Hilali hadi kiasi cha deni linalodaiwa litakapolipwa huku akidai kuwa uongozi wa mgodi umekaidi amri halali ya kusitisha kazi zote mgodini hapo lakini chakushangaza maofisa ukaguzi wa TRA walipofika katika eneo hilo siku moja baada ya kuufunga mgodi walikuta baadhi ya kazi zikiendelea kama kawaida kinyume na maagizo yao.

Naye kaimu meneja wa kitengo cha uzalishaji katika mgodi huo Bw.Bader Seiph alipoulizwa kwanini amekiuka amri ya kusitisha uzalishaji na kuruhusu magari kuendelea kusomba kifusi chenye madini ya almasi alikataa na kudai hakuna kazi inazoendelea mahali hapo lakini maofisa wa TRA walipofuatilia walikuta magari sita yakiendelea kufanya kazi na kulazimika kuyakamata na kuyapeleka katika yadi ya TRA iliyopo mjini Shinyanga kwa hatua zingine zaidi.

Nao baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo wamelalamika kuhusu kufungwa kwa mgodi na kuuomba uongozi wa mgodi kulipa deni hilo mapema iwezekanavyo kwakuwa hali hiyo itawafanya kuishi maisha ya shida huku meneja wa TRA tawi la Shinyanga Bw.Ernesti Dundee akidai kuwa zoezi la kuwasaka wakwepa kodi ni endelevu hivyo makampuni mengine yalipe kodi ya serikali kabla hayajafikiwa.

Chanzo: ITV
 
Almasi haina hasara kodi hawataki kulipa mbona ni chenji tuu iyo ni kwa Muda gani huo..wakati wao kipande kidogo tuu wanauza Hela ndefu Hong Kong..hawa wachimba Madini Nani yupo Nyuma yao ni Nchi gani watachimba wasilipe kabisa..kwani lazima yachimbwe si yaachwe kama kuna watu wanataka wachukue Bure..Hayaozi hayo..
 
Huo mgodi una milikiwa na mfadhiri na mwwnyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga. Kwa wale wasio fahamu bwana Hilal mmiliki wa huo mgodi anamiliki na kampuni ya kuuza mafuta iitwayo Phantom. Kampuni hiyo ya mafuta inauza mafuta yaliyosamehewa kodi kutoka kwenye huo mgodi. TRA shinyanga wanalijuwa hili siku nyingi kwani New Almasa ni mgodi mdogo kuliko Mwadui lakini fuel consumption yake ni mara mbili ya Mwadui....
 
Natamani sana jpm apewe haraka uenyekiti wa ccm ili atumbue majipu kama bwana Hilal, m/kiti ccm Shy. Matajiri hawa walinunua vyeo ndani ya ccm ili kuwa salama katika harakati zao za kufanya ufisadi. Katika hili nawalaumu sana jk, el na kundi lao la wanamtandao ambao wamekifikisha chama hapa. Halafu kuna watu walitaka el awe rais, kweli? Watanzania lazima tuwaelewe kinaga ubaga wale wote wanaotafuta uongozi wa taifa letu.

Hata hivyo namshukuru jk kwa kujitenga na wanamtandao nafikiri baada ya kung'amua ubaya wa kundi hilo na kufanya maamuzi kinyume na mapenzi yao. Sasa namwomba amkabidhi rungu la uenyekiti wa ccm jpm, ili akirudishe chama kwa wenyewe wakulima na wafanyakazi baada ya taswira ya chama kujeruhiwa na matajiri kama akina Hilal. Fanya hima rais mstaafu jk.
 
Phantom mmiliki wa mgodi huu!! Ndo alikuwa mmilika wa Savannah Plains Schools sasa ukiconect Dots..... Mhhh
Kumbe lisemwalo lipo?? Walisemaga shule na mgodi wamiliki wako Msoga
 
Huo mgodi una milikiwa na mfadhiri na mwwnyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga. Kwa wale wasio fahamu bwana Hilal mmiliki wa huo mgodi anamiliki na kampuni ya kuuza mafuta iitwayo Phantom. Kampuni hiyo ya mafuta inauza mafuta yaliyosamehewa kodi kutoka kwenye huo mgodi. TRA shinyanga wanalijuwa hili siku nyingi kwani New Almasa ni mgodi mdogo kuliko Mwadui lakini fuel consumption yake ni mara mbili ya Mwadui....
hawa jamaa bado wanaona wengine watumwa sijui mpaka lini? mtu unapata mihela lakini hulip kodi ili watu wapate japo aspirin hospitalini hataki. tukisema warudi huko walikotoka wanasema ubaguzi. tangu lini mwafrika kumbagua mtu kwa jinsi tulivyopigika tangu kale.
 
Huo mgodi una milikiwa na mfadhiri na mwwnyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga. Kwa wale wasio fahamu bwana Hilal mmiliki wa huo mgodi anamiliki na kampuni ya kuuza mafuta iitwayo Phantom. Kampuni hiyo ya mafuta inauza mafuta yaliyosamehewa kodi kutoka kwenye huo mgodi. TRA shinyanga wanalijuwa hili siku nyingi kwani New Almasa ni mgodi mdogo kuliko Mwadui lakini fuel consumption yake ni mara mbili ya Mwadui....
hii nchi imeoza...hawa CCM wanatupeleka pabaya sana TZ........
YAANI KILA JAMBO LA KULETA MAENDELEO KWA WANANCHII
wamejibinafsishia na kumiliki ccm
 
Phantom mmiliki wa mgodi huu!! Ndo alikuwa mmilika wa Savannah Plains Schools sasa ukiconect Dots..... Mhhh
Kumbe lisemwalo lipo?? Walisemaga shule na mgodi wamiliki wako Msoga
Mirija ya msoga inakatwa pole pole!!!hilo ni kweli kabisa december nilikua shinyanga wenyeji wakaniambia ni mali familia msoga
 
Kwanza huo mgodi una jina la kiarabu, kwa nini??? Inabidi kama hawataki kutumia majina ya kina mkwawa basi walipe
Ndugu wee wa ajaabu sana!! Nchi nzima ina majina ya KIARABU !! ati mgodi una jina la kiarabu?!! una akili finyuuuu!!
Majina yote yaliyomo nchini yametokana na kiarabu (miji/wakazi/lugha/nk..nk) Tafuta neno la kuhoji ktk uzi... siyo kukurupuka!
 
Mimi skumaanisha saaana kama ulivyonijibu.
 
Kwanza huo mgodi una jina la kiarabu, kwa nini??? Inabidi kama hawataki kutumia majina ya kina mkwawa basi walipe
Hata ikulu ya tz ina maneno ya kiislam (kiarabu) ww una ajabu mgodi?
Na kina kuuma nini ww mgodi wa muarabu kupewa jina la kiarabu?
Haikuumi ziwa victoria kupewa jina la mzungu?
Wakati ziwa lipo tanganyika lakini jina la ziwa la mzungu?
 
Back
Top Bottom