beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,367
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaandaa mpango maalum kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma.
Dk. Kijaji ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoani humo na kutoa tathmini ya ziara yake aliyoifanya katika mpaka wa Tunduma na Zambia.
Amesema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato yake kutokana na biashara hiyo.
Dk. Kijaji amesema serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjari na kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa kodi.
Chanzo: EATV