TRA yakamata mitambo ya Dowans

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Nimesikia habari punde kutoka TBC ! kuwa TRA, kupitia majembe Auction Mart, imekamata mitambo ya Dowans kwa madai kuwa haijalipa kodi ya zaidi ya Sh bilioni 9.
 
11_09_urzh2h.jpg

Ofisa wa Kampuni ya udalali ya Majembe Auction Mart Emmanuel Wambando akionesha mitambo ya Kampuni ya Dowans ambayo kampuni hiyo inaishikilia kufuatia idhini ya Mamlaka ya mapato nchini (TRA) inayoidai kodi ya zaidi ya sh Bilioni 9.120. Jana Majembe wamefunga kwa kufuli eneo hilo la mitambo iliyopo Ubungo Dar es Salaam.(Picha na Mroki Mroki).
VIDEO | PODCASTS VIDEO ZAIDI | MAONI
 
Nimesikia habari punde kutoka TBC ! kuwa TRA, kupitia majembe Auction Mart, imekamata mitambo ya Dowans kwa madai kuwa haijalipa kodi ya zaidi ya Sh bilioni 9.

Fisadi Rostam kama kashindwa kulipa kodi basi afilisiwe na kitakachopatikana kikalipe hilo deni lake.
 
Lakini turudi kwenye ukweli, Deni hilo lote kwa kipindi ambacho hawa waheshimiwa wamekuwa kwenye operation hawakuwahi kudaiwa?

kama waliwahi kufanya hivyo je ilishindikana kuchukua hatua hizo mapema nakusubiri mpaka wanapotaka kutoweka?
 
ushabiki mwingine bana...

Huu si ushabiki bali ni kutetea maslahi ya Taifa. Kwenye nchi za wenzetu unaposhindwa kulipa kodi hata nyumba unayoishi itauzwa ili kufidia deni lako la kodi. Kwanini na Tanzania tusiwe na utaratibu huo ili kuwazuia watu wanaokwepa kulipa kodi wasifanye hivyo!? Ukijua nyumba yako inaweza kunyang'anywa ili ulipe deni lako la kodi basi usanii wa watu kama huyu fisadi utatoweka kabisa nchini.
 
Jioni ya leo TRA wakiongozana mawakala wao Majembe walifika kuliko mitambo ya Dowans wamefunga kufuli zao na kukamata magari ya wafanyakazi wa Dowans,pia waliagiza mitambo isiuzwe wala isihamiswe. Cha ajabu nasikia haupita muda walirudi tena wakiwa wameloa jasho na kufungua kwa amri kutoka Ikulu. ikulu ina ubia na Dowans??!!
 
Kwani TRA walikuwa wapi mpaka kodi inafika kiasi hicho na bado tuna kamishna mkuu bwana Kitilya akilipwa mamilioni si kwa kazi ipi hivi kodi wanaolipa ni watu wadogo tu,hao Dowans wenyewe wanalipwa mapesa kibao na ni ajabu na aibu kuwa wanaachia kwa kutolipa kodi hadi kufikia kiasi hicho swali watoza ushuru wetu walikuwa wapi au ndo kumuogopa Godfather wa Mafisadi
 
Tehe nimefurahi kumwona yule jamaa msimamizi wa mitambo aliyekataa kutaja jina lake akasema mkawaulize wenye mitambo yeye si msemaji wa kampuni, anaitwa mr mwandenga, ni engineer, miaka ya 90 alikuwa tanesco naona kumbe alifuata green pastures kwa fisadis
 
Mwaka huu tutashuhudia salakasi kama za wachina. Kwa kweli tunakazi kubwa ya kufanya. Mafisi wametushika pabaya Tanzania inapumlia mashine. Mkuu wetu wa kaya Kimya mafisi adi wanafanya kazi. Akisikika ni kulalamika na porojo tu
 
Jioni ya leo TRA wakiongozana mawakala wao Majembe walifika kuliko mitambo ya Dowans wamefunga kufuli zao na kukamata magari ya wafanyakazi wa Dowans,pia waliagiza mitambo isiuzwe wala isihamiswe. Cha ajabu nasikia haupita muda walirudi tena wakiwa wameloa jasho na kufungua kwa amri kutoka Ikulu. ikulu ina ubia na Dowans??!!

mbona mnatuchanganya? majembe wamezuia mitambo au ikulu imekuja juu?
 
Kazi kweli kweli! Mbona sinema! Au ndiyo kufuata mapendekezo ya Zitto! Si waseme tu wanaitaifisha...!!! Tusubiri tutajionea...!!
 
Hawas tra ni mapumbafu sana tena sana...hat hii kuitoa hadharani jamani yawezakana wameomba hongo ya billion jamaa wakwachomolea..kwa mantiki hii yale makampuni ya migodi si yanavuna bure jamani.....
Mungu ibariki tanzania
 
Changa la Macho Hilo!!!!!!!!

Chama cha Mafisadi hawajui sheria za nchi hii. Ni hivi karibuni tu mbunge wa upinzani alisema hiyo mitambo itaifishwe. Akaja waziri husika akasema kuwa Tanzania haina sheria ya kutaifisha mali za watu!

Mpo hapo?

Leo tunaambiwa TRA wanataifisha mitambo kwasababu kodi ya 9.1Bil haijalipwa.

Swali ni kwamba, siku zote TRA walikuwa wapi?

Mkuu wa Tanesco angekubaliwa ombi lake la kununua hiyo mitambo mapema mwaka huu, hiyo kodi ingelipwa lini?

Mpo hapo?

Hilo ni changa la macho tu. Serikali itachukua hiyo mitambo halafu watamuuzia mtu hapa bongo.

Guess who is going to buy? Guess who is going to get a new contract to supply power into national grid?

We need to smell the coffee if not the roses.

Lets wait!
 
Duh mafisadi wanajitahidi kuwahadaa watanzania but ngumu, watanzania si mabwege tena!!!!!!!!!!!!!!!
 
:confused:
Bhayanda,

Nisha waulizeni hapo kwa JF haya maswali:

1: Nini maana ya IKULU??
2: katika hii mihimili 3 Bunge, Mahakama, Serikali ------ IKULU inatokea wapi na kuwa na mamlaka??
3: IKULU ndio serikali?????

Maana matamko mengi yamenitatanisha hapa;
week chache zilizo pita Kauli ilitoka IKULU rais kaaagiza mtambo wa IPTL uwashwe haraka sana???mmmh nkagutuka
Gafla ndani ya siku sita Meli imeishatua nanga Dar Es Salaaam jamaaaani.

Nambo niambiwe anu mnipe ndo ndo za mgawanyiko wa Kikazi kati wafanyakazi waliko IKULU na wale wa wizara husika na ni wapi tamko la serikali hutakiwa kutole na ni wapi IKULU yapaswa kutoa tamko ktk hali gani??

TRA nayo ni ya kuchunguzwa jamani au nayo yapewa makali ya kunyoa ikinyoa nayo huambiwa weeeeeee alaaaaaa wapenda kunyoa na visivyo nyolewa???? Au Wapi kanuni na sheria za kiutendaji za kuilinda TRA katika utendaji kazi wake??

Kuna Taasisi nyingi zinashindwa kuundwa makusudi kabisa wakijua fika viongozi wetu watarumbana tu pale mamlaka, Sheria za kiutendaji zitakapo undwa na kuiruhusi iyo taaasisi ifanyekazi itakula kwao, sasa wanaamua kutuburuza wajisikiavyo na kutoa kauri vyovyote wajiskiavyo; Tukihoji kweli watupe Takwimu kweli Dowans wanalipa Kodiiii? Nakama hawalipi Iyo kampuni inafanya kazi gani humu nchi???? Kama ina Kesi mbona hiyo kesi haiiishi na haina au haijulikani aye imiliki iyo kampuni??? Mahaka zetu zahukumu hewa au???
 
Back
Top Bottom