TRA yaikadiria ACACIA deni la Tsh. Trilioni 425.4 kama Malimbikizo ya Kodi

Hahaha...Magufuli taratibu anaifanya nchi ionekane inaongozwa na wendawazimu, aibu jamani dah!
 
Serikali ya Tanzania imesema kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu yenye makao yake nchini Uingereza Acacia inadaiwa na walipa kodi dola bilioni 180 ,kama malipo ya adhabu na riba, kulingana na taarifa ya kampuni hiyo.

Takwimu hiyo ni kulingana na ufichuzi uliofanywa na tume mbili za rais kuhusu sekta ya uchimbaji madini.

Kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Awamy deni hilo linalodaiwa Acacia linasimia mapato yaliopatikana ambayo hayakutajwa kutoka kwa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi katika kipindi cha mwaka 2000 na 2017.

Acacia imepinga madai hayo na kusema kuwa inatafuta njia mbadala

Uchunguzi uliofanywa na tume hizo za rais uliishutumu Acacia kwa kufanya operesheni zake kinyume cha sheria na kushindwa kulipa inachodaiwa.

Acacia ambayo ndio kampuni kubwa inayochimba madini nchini humo ,imesisitiza kuwa imekuwa ikitangaza mapato yake.


Chanzo: BBC swahili

Katika mkutano wa hadhara siku ya Ijumaa rais John Magufuli alitishia kufunga migodi yote ya dhahabu nchini humo iwapo kampuni za kuchimba madini zitachelewa kufanya mazungumzo na serikali yake yanayolenga kutatua madai ya ukwepaji kodi.
 
Napenda walipe lakini tukienda kwenye mahakama za nje historia inaoenesha atutoboi kutokana na makubaliano au mikataba corrupt
Pia tamko hilo ni la ipande mmoja ambao ni tz tudubiri accacia na mtu wa kati ambaye ni mahakama za kimataifa

Nb:.sheria ziheshimiwe kwa wote
 
Kuna watu wamelifikisha taifa hapa tukapata hasara ya fedha kama hizo kwanini mpaka sasa awajapelekwa mahakamani kupata hadhabu yao kwa kulisababishia hasara taifa wananchi tunachotakiwa ni kuiadhibu ccm 2020 kwa kutufikisha hapa
 
Mpaka leo ACACIA wanadai Serikali ya JPM imegoma kuwapa copy za zile report mbili. Kwa nini? Badala yake JPM na watu wake wapo busy kuissue invoices. Huu ni uzwazwa. Report zote ziwekwe mezani zijibiwe kwa hoja. Wakishindwa, watupe chetu. Hata kama wote tunataka zile Noah zetu, lakini lazima tuzipate kihalali. Kwa kodi ile naona sasa sio tena Noah. Tutavuta Verrosa.
 
Back
Top Bottom