TRA yaeleza chanzo cha deni la trilioni 424 inazoidaiwa Acacia

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema kuwa deni la Tsh 424 trilioni inayoidai Migodi ya Bulyanhulu Gold Mine (BGML) na Pangea Minerals (PML) inayoendeshwa na Acacia limekokotolewa na wataalamu wa kodi waliobobea waliokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati mbili za kuchunguza makinikia zilizoteuliwa na Rais Magufuli.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na gazeti la MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa TRA, Gerald Mwanilwa alisema, “Deni la Acacia halikuja kibahati mbaya, lilikokotolewa na wataalamu wabobezi wa masuala ya kodi tangu (BGML na PML) walipoanza kukwepa kodi hadi tulipobaini jambo ambalo limesababisha deni kuonekana kubwa.”

Afisa huyo alisema kwamba, wote wanaodhani TRA imezikomoa kampuni hizo kwa kuzipa deni hilo, wanakosea kwa sababu deni hilo limetokana na malimbikizo ya ukwepaji kodi.

Taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Acacia baada ya kupata madai hayo ya TRA ilionyesha kuwa deni hilo la USD 190 bilioni, BGML wanadaiwa USD 154 bilioni na PML wakidaiwa USD 36 bilioni.


Katika USD 190 bilioni, USD 40 bilioni ni malimbikizo ya kodi na USD 150 bilioni zikiwa ni riba na faini kutokana na kukiuka sheria.

Chanzo: Swahili Times
 
Sasa siku zote walikuwa wapi!wanatakiwa TRA washitakiwe pia kwani walikuwa hawafanyi ukaguzi kwa nini sasa!na kwa nini hawajapelekwa mahakamani au kufungiwa milango kama kwenye vibiashara vyetu.Vitu vingine haviingii akilini hata kidogo
 
Huwezi kujua kiwango cha Corporate Tax kinachoaswa kulipwa kwa kuangalia tu Mapato bila ya ku consider Gharama za kuzalisha hayo Mapato!

Aibu ile ya TRA kimataifa imenifanya na Umri wangu nipende kusikiliza yake Maneno ya Wimbo 'Bongo bahati mbaya' japo Sijui Maana yake kwa ufasaha wala Nani kaimba!

Miaka yote wamekuwa wakitoa Certificate of clearance kwa Acacia Halafu unatumia report ya wale ma Prof Osoro na Mruma Makomunist ku charge Kodi ya kufikirika!

Wale ma Prof wamekishushia Heshma sana Udsm
 
Kama ndio hao waliomkokotolea Diamond tumepigwa, hawajui hesabu, sababu nakumbuka Diamond walimdai milion kama 100 hivi, kafanya biashara gani haijurikani.
 
Ukiona TRA wanaanza kujikosha ujuwe walipokokotoa hawakutumia misingi ya kukokotoa kodi.. Kwani chanzo cha kukokotoa kodi si makabrasha ('documents')? Wao kwa nini watumie Ripoti za Wajumbe wa Kamati? Si wangetumia Ripoti za Uzalishaji ('production reports')?
 
Kama ndio hao waliomkokotolea Diamond tumepigwa, hawajui hesabu, sababu nakumbuka Diamond walimdai milion kama 100 hivi, kafanya biashara gani haijurikani.
Pamoja na mziki, pia Diamond anauza karanga siku hizi.
 
Back
Top Bottom