Kwa muda mrefu sasa TRA wamekuwa wakituaminisha kuwa ni taasisi inayo fanya kazi kwa viwango vya hali ya juu katika kutekeleza majukumu yake, hadi kupewa cheti cha ubora cha ISO 9001:2008.
Cheti cha ubora cha ISO 9001: 2008 kinahusu ubora wa mifumo ya uendeshaji wa taasisi (Quality Management System) huusisha pamoja na mambo mengine, mfumo wa uongozi wa taasisi (organization structure), michakato (Processes), mifumo ya taarifa (Information System).
Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, tumeshuhudia madudu mengi, yaliyosababisha upotevu wa fedha nyingi za umma, hali ambayo inathibitisha kwamba TRA kama taasisi haijajipanga kimkakati na haina ubora kuanzia mfumo wa utawala, michakato (processes) yake na hata mifumo ya taarifa (IT systems) jambo ambalo linasababisha mabilion ya fedha za umma kupotea.
Kufuatia madudu haya yaliyojitokeza napendekeza kwamba ISO wawanyang'anye TRA cheti cha ubora, hadi pale TRA watakapo jipanga upya.
Tunafahamu kuwa kwa sasa TRA wameongezewa majukumu ya kukusanya mapato ambayo si ya kodi, nchi nzima. Je kwa mwendo huu wataweza kufanya kazi hii kwa ufanisi.
Nashauri kwamba, TRA waangalie mifumo yao upya, ikiwa ni pamoja na ku review business processes na IT systems.