TRA wanyang'wanywe cheti cha ubora cha ISO 9001:2008

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,870
4,264
Kwa muda mrefu sasa TRA wamekuwa wakituaminisha kuwa ni taasisi inayo fanya kazi kwa viwango vya hali ya juu katika kutekeleza majukumu yake, hadi kupewa cheti cha ubora cha ISO 9001:2008.

Cheti cha ubora cha ISO 9001: 2008 kinahusu ubora wa mifumo ya uendeshaji wa taasisi (Quality Management System) huusisha pamoja na mambo mengine, mfumo wa uongozi wa taasisi (organization structure), michakato (Processes), mifumo ya taarifa (Information System).

Tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, tumeshuhudia madudu mengi, yaliyosababisha upotevu wa fedha nyingi za umma, hali ambayo inathibitisha kwamba TRA kama taasisi haijajipanga kimkakati na haina ubora kuanzia mfumo wa utawala, michakato (processes) yake na hata mifumo ya taarifa (IT systems) jambo ambalo linasababisha mabilion ya fedha za umma kupotea.

Kufuatia madudu haya yaliyojitokeza napendekeza kwamba ISO wawanyang'anye TRA cheti cha ubora, hadi pale TRA watakapo jipanga upya.

Tunafahamu kuwa kwa sasa TRA wameongezewa majukumu ya kukusanya mapato ambayo si ya kodi, nchi nzima. Je kwa mwendo huu wataweza kufanya kazi hii kwa ufanisi.

Nashauri kwamba, TRA waangalie mifumo yao upya, ikiwa ni pamoja na ku review business processes na IT systems.​
 
Accreditation yoyote haitolewi kama zawadi, hutolewa baada ya kujengwa kwa mfumo wa kiundeshaji ambao huakisi matakwa ya standard hiyo. Taasisi hufanyiwa ukaguzi " announce & and unannounced" inspection by the owners of the scheme to ascertain its compliance to the standards prior certification decision is made. To maintain their certification annual audits are conducted for those who pass certification audit.. TRA is not an exceptional to this standard, time will just tell and it might end up loosing its accredittion
 
Mkuu hii hoja yako mara kadhaa mimi nimewahi kuifikiria kwa taasisi zetu mbali mbali zikiwemo TRA, TCRA,PPF na mashirika mengine. Pamoja na mambo mengi mazuri ya ISO 9001:2008 Lakini TCRA na TRA zinachangamoto nyingi sana, mfano TCRA imeshindwa kuyadhibiti makampuni ya simu yanatufanyia unyonyaji wa hali ya juu, hapa pia ninailaumu FCC Fair Competition Commission yaani kama hawapo Tanzania
 
Back
Top Bottom