Copy
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 1,021
- 1,258
Kesho nikitulia itabidi nilete baadhi ya mambo yanayonitatiza ili unipe msaada mkuu.
Huyu Mheshimiwa anaweza akawa haelewi kodi na namna ya kulitatua hili au Mamlaka ya TRA wanadai kodi ambayo si halali either kwa makusudi au kwakuwa hawana taarifa sahihi za mlipa kodi wao. Audit inapofanyika, TRA hutumia evidence walizonazo kutoa makadirio kama watakuwa wamekukagua. Wewe jukumu lako ni kujitetea kuwa TRA hamkupitia kitu moja mbili tatu wakati mnaandaa hesabu zenu. Una nafasi ya kufanya hivyo ndani ya siku 30 (siku za pingamizi kama ulikaguliwa na wakatoa assessment). Huyu kapewa nahisi ni Demand Notice. Ambayo unaijibu ndani ya Muda waliokupangia au unaomba Muda wa kujibu.
Ukionewa unaweka pingamizi kwa Commissioner, Commissioner akikuonea unaenda Tax Revenue Appeals Board (TRAB), inatoa maamuzi, ukionewa unaenda TRAT (Tax Revenue Appeals Tribunal) ukionewa na hapo unaenda Mahakamani.
Pia kuna muda watu hawajui Sheria ndio maana wanajikuta wanapigwa kodi kubwa. Mimi nilikuwa na mteja wangu mmoja wa Oil and Gas nikiwa Consultant wa Kampuni fulani alipigwa Kodi 9billion mpaka nikaduwaa.
Tukapambana tukaweka vielelezo akaishia kulipa Million 230 tu.
Jamani huko TRA weledi ni Mdogo sana wa Watendaji lakini pia kuna Tatizo la Walipa kodi kutokujua Sheria.
Natamani Siku humu ndani nifunguke kuhusu Kodi, Changamoto zake na Pia Madhaifu ya TRA na Madhaifu ya Walipa kodi na Ninyi cha Kufanya.
Mkiniruhusu naweza weka Uzi mmoja wa hayo yote hapa. Ila pia mwenye Maswali ya kodi ananiuliza hapa (nisiyoyajua naenda kuwataftieni majibu). Ahsanteni.