TRA wanavunja rekodi ya mapato: Serikali haina pesa hapo vipi?

serikali ya wezi hiyo naona hela za kuiba zimepungua wanajaribu kuwahadaa watanzania ili waibe hata kile kile kidogo kilichopo kweli ufisadi umekithiri serikali ya kikwete
 
wana set target ya kukusanya 5 wakati wana uwezo wa kukusanya 50, so wakikuambia wamevuka lengo kwa kukusanya 10 kichwa maji kama wewe utawapongeza wakati wenzako wamepiga 40 wanasubiri mwezi wa kumi nambili wanaenda kupiga mbege moshi. usicheze kabisa na wachaga wale!
 
Njii hii mtashangaa sana! Na bado! ATCL kwishney, TRL kwishney, shule za sekondari za serikali hata zile zilizokuwa zinaheshimika miaka ya nyuma nazo kwishney! kila kitu kwishney!
 
Ni swali zuri sana!

Majibu yako makao makuu na vyanzo vyake vya utawala!


Kazi ipo kweli kweli!
 
Msamaha wa kodi nao ni chanzo cha upotevu wa mapato!

wa kuwasamehe kina jah pipo? Kuwasamehe kina ra? Kina blandina? Tuacheni kujitetea kwa majibu mepesi,huu ni uzembe na uhujumu uchumi. Msamaha wa kodi ulitolewa kwa mashirika yanayotoa huduma bure/at subsidized cost kwa wananchi. Watu kila siku wanatulangua aafu tunawapa msamaha wa kodi! Serikali ya jk ni mbovu sababu ya ubovu wa rais. Ameingiza matapeli kwenye serikali sasa kila sekta vimemo. Hospitali,tra,bot,tpa unadhani tutafika? Haiwezekani wewe kama kiongozi wenzako waache hazina kubwa aafu kwenye utawala wako ukose hata fedha za mishahara! Jk nazi tu!
 
Nchi ya walalamikaji nilimsikia mkubwa wa TRA akisema wangekusanya zaidi kama isingekuwa vimemo wanavyolazimishwa watoe misamaha ya kodi unajuwa wamesame kwa kiasi gani kwa ripoti ya CAG ( 18%)
Sasa ndugu yangu embu tafiti uone nani wamesamehewa makampuni yote ambayo vigogo na watoto wao wana ubia na makampuni hayo ,kazi ipo kweli kweli

Hivi vimemo huwa ni balaa kwa uchumi wa nchi yetu. Nasikia enzi zile ATC ikifanya safari zake hadi London kuna watu walikuwa wanasafiri kwa vimemo kutoka DAR hadi London na ndo mwanzo wa kulimaliza shirika letu la ndege.
 
Wala hainiingii akilini, kuikubali lazima uwe na matatizo ya kifikra. Kwamba pesa iko tena wanavunja rekodi ila wale ambao kodi hukusanywa na kupekwa kwao HAWANA PESA? We are lacking strategists in this country!!!!!!
Watz huwa tunalishwa data tu na kuridhika. Viongozi wetu wanatuelewa vizuri sana. Ndiyo maana utamsikia rahisi kikwete anasifia uchumi unaojengwa na sirikali yake kwamba unakua kwa kasi kuliko nchi yoyote kusini mwa jangwa la sahara wakati wanachi mitaani hata mlo mmoja wanabahatisha tu.
 
Hilo swali lilipaswa kumtoa Mkullo nje ya uwaziri. Hilo swali litawatoa ccm ktk "milki" yao miaka michache ijayo. Hilo swali JK na serikali yake hawataweza kulijibu ktk kipindi chote cha muhula wake uliobaki. Lakini hili swali ni lazima lijibiwe haraka na kwa usahihi.......so lazima waanchi waamke
 
Kuna genge la magamba linafanya linavyotaka hapa nchini kwetu!! Ni juu yetu kuamua kusuka au kunyoa ili kubadili hii tabia.
 
Back
Top Bottom