crispaseve
Member
- Sep 27, 2011
- 16
- 6
Nimekuwa nawasaidia watu ku apply Ajira kwa njia ya tovuti ya utumishi wa umma lakini Hiki kigezo cha kutoa copy vyeti na kupeleka kwa mwanasheria a certify copies zako halafu ndiyo upload kwa njia ya tovuti ya ajira utumishi wa umma siyo kibaya. Bado najiuliza mwanafunzi aliyeoko kijijini anawezaje kufanya maombi kwa njia hii online ambayo huku mjini tuu asilimia 80 ya internet cafe network inasumbua mana sio wote wenye laptop na bado hata ukiwa na laptop stationary itakuhusu kuscan tuu. Je mwenye jukumu la kuthibitisha cheti ni mwanasheria na muhuri wake au chuo/nacte waliokupa cheti mana tumekuwa tunawaongezea gharama waombaji ikiwa hata ajira zenyewe hawana. Labda Utumishi/TRA waseme wanahitaji watu wachache ndyo wakaweka vigezo vingi mana hakuna haja ya kukataa njia ya posta ambayo tungepata waombaji wengi. Tunapenda kuwa digital lakini mazingira yetu hasa mikoani bado tuko analog aisee!