TRA wanampango gani Vijana kwakuweka vigezo vigumu kufanikisha kutuma maombi ya Ajira?

crispaseve

Member
Sep 27, 2011
16
6
Nimekuwa nawasaidia watu ku apply Ajira kwa njia ya tovuti ya utumishi wa umma lakini Hiki kigezo cha kutoa copy vyeti na kupeleka kwa mwanasheria a certify copies zako halafu ndiyo upload kwa njia ya tovuti ya ajira utumishi wa umma siyo kibaya. Bado najiuliza mwanafunzi aliyeoko kijijini anawezaje kufanya maombi kwa njia hii online ambayo huku mjini tuu asilimia 80 ya internet cafe network inasumbua mana sio wote wenye laptop na bado hata ukiwa na laptop stationary itakuhusu kuscan tuu. Je mwenye jukumu la kuthibitisha cheti ni mwanasheria na muhuri wake au chuo/nacte waliokupa cheti mana tumekuwa tunawaongezea gharama waombaji ikiwa hata ajira zenyewe hawana. Labda Utumishi/TRA waseme wanahitaji watu wachache ndyo wakaweka vigezo vingi mana hakuna haja ya kukataa njia ya posta ambayo tungepata waombaji wengi. Tunapenda kuwa digital lakini mazingira yetu hasa mikoani bado tuko analog aisee!
 

Attachments

  • utumish.jpg
    utumish.jpg
    32.4 KB · Views: 143
Kwa nchi yetu bado sijaona umuhimu wa utandawazi hasa kwenye mambo kama haya ambayo yanagusa maendeleo ya Taifa
 
Kwa nchi yetu bado sijaona umuhimu wa utandawazi hasa kwenye mambo kama haya ambayo yanagusa maendeleo ya Taifa
Ni bora wangetoa option zote tuu hata wale walioko vjijini wawezeze kushiriki suala hili mana ajira ni tatizo la taifa sio mjini tuu
 
Kuongezeana usumbufu na kutengeneza ulaji kwa watu wengine.
Sasa kugonga muhuri kunasaidia nini?
Kama mtu alifanya forgery ya cheti bado mwanasheria hana uwezo wala vyombo vya kutambua forgery.

Hii nchi inazidi kupiga hatua kinyume nyume

Nothing is easier than blaming others for your own problems
 
Back
Top Bottom