TRA wanajipa sifa wasizosatahili

TRA wanajipa sifa wasizosatahili

Mandesy

Senior Member
Joined
Mar 22, 2018
Posts
115
Reaction score
125
Nimeona taarifa ya TRA kuhusu mapato ya mwezi Septemba. Kwa nasibu, Mkurugenzi wa TRA amesema wamekusanya shilingi trilioni 1.7, kiwango ambacho hakijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mamlaka hayo mwaka 1995.

Kwanza.. wakati TRA inaanzishwa, uchumi haukuwa na ukubwa wa kukusanya fedha kama hizo hata bilioni 150 zilikuwa ni nyingi sana

Pili, Mapato ya serikali yamekuwa yakiongezeka kwa kiwango cha kupungua (increasing at decreasing rate) kwa miaka ta karibuni kuanzia mwaka 2014 na kuendelea.

Tatu. TRA hawajasema mapato hayo yametokana na kodi na mapato yasiyo ya kodi.. walichofanya ni kutufunika blanketi ili kujipa sifa. Hawajasema malimbikizo yaliyokusanywa yalikuwa kiasi gani?

Nne. Kukua kwa mapato nadhani sio jitihada binafsi, bali ni kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi.

Tano. Iweje waseme kodi imekusanywa saa sita kabla ya kutangazwa.. database wanasoma hadi usiku?

Sita. TRA iache kujinasibu, bali ifanyekazi iliyotumwa na taifa ya kukusanya kodi, sasa wanapoanza kujipambapamba wakati hawajafikia hata lengo huu ni ukuda na kujipendekeza.

Saba. Tuwapongeze walipa kodi nikiwemo na mimi ambaye nakatwa zaidi ya milioni 6 kila mwaka kwa ajili ya PAYE ambayo ni mishahara ya waalimu kumi au mishahara ya polisi mmoja ya mwaka mzima.



Otherwise, TRA waache kujinasibu na sifa feki.. ndo zile sifa za kijinga

Nawakilisha..Povu linaruhusiwa kutoka kwa Mataga!!!! Matege!!!!!
 
Naona Desemba 2017 walikusanya Shs 1.66 trilion
TRA: Makusanyo ya Mwezi Dec 2017 yamepanda hadi trilioni 1.66 sawa na ongezeko la ukuaji wa 17.65%
 
Ulichoandika ni sahihi kabisa hayo mapovu Kwa hawa malofa achana nayo...
 
Back
Top Bottom