Tra tra tra tra

Mmwaminifu

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
1,129
302
Heshima zenu wakuu.

Nimeamua kulipa kodi kwa hiari ila nasikitika kwamba TRA wameniangusha.

Tangu saa tatu asubuhi niko TRA dodoma hapa. Nalipia motor vehicle ila nasikitika MAXIMALIPO wanasema mtandao wa TRA unasumbua. Tangu nifike hapa wameweza kulipa watu wanne tu.

Kulipia kwa njia nyingine (bank, mpesa) wanasema ndio worse. Majibu yanachelewa sana na hela inachelewa sana kuonekana kwenye mtandao.

Kama leo watu wachache tu, network inasumbua hivi. Wakija na wa pikipiki wanaobadilisha registration numbers si ndio network itacollapse kabisa?

Naomba kuwasilisha.
 
unakusanya mapato ya nchi kwa network finyu, kwa nini msiboreshemkonga wa taifa mliotandaza nchi nzima!?
 
Yaani. Nilidhani kwa kutumia haya ma mitandao itaongeza ufanisi badala yake imekuwa kero sana kwa walipa kodi. Siku yangu yoooote inaishia kwenye foleni.
 
Back
Top Bottom