TRA Tanga, nihurumieni jamani

Kwani ukifunga biashara ukaanza kuuza vitumbua watakuja kukuuliza...watakupatia wapi...

Vitumbua nayo ni biashara kama biashara zingine, tatizo lako unaitazama kwa jicho la dharau ndio maana wengi wanabaki walipo,itakuwaje hapo baadae mtaji wako utakuwa mkubwa na unataka kuiendesha biashara yako kisasa ( Kwa mf:Omar Ndama Bites and Snacks) jambo linalohitaji ufuate taratibu za kiserikaliunadhani hapo TRA utawakwepea wapi?ndugu huyu hana budi kwenda TRA kama kuwaelezea kuwa anafunga biashara kama alivyokwenda kuwaambia anaanzisha biashara.Huo ni ushauri tu kukubali au kuukataa ni juu yake.
 
Wakuu HV nikienda kuwaambia biashara imenishinda watanielewa kweli au bado watataka niwalipe nimekosa aman, hii nchi yetu jaman inakoendea mbona ....
Nenda waambie nimeshidwa kulipa hiyo kodi naona sitaimudu kulingana na aina ya biashara mtaji wake na gharama za uendeshaji, kwa hiyo umeamua kuifunga, pia ingekua vizuri ukaonana na meneja wa tawi au yule anaepitisha kiwango cha kodi kilichokadiriwa na maafisa wa chini yake unaweza kuongea nae ukamuomba akakupunguzia,
Angalizo, kama uliwaambia kua ushafungua biashara lazima uwalipe kwa kipindi ulichofanya biashara, kama ndivyo andika barua mapema ya kufunga biashara yako hata kama utakua hujalipa deni ili kukwepa deni kuongezeka kila mwezi.
 
Hii nchi ukijifanya mstaarabu sana ndo unaumia,wajanja wajanja ndo wanapeta
 
Hiyo elfu50, ni asilimia 10 ya pango ya mwaka mzima. Hapo bado cjaanza hata kutoa mapato yao
Dada jaribu kutafuta information kwa waelewa wa kodi. Hio ya 10% ni withholding tax kwenya pango, tena kuna additional 1% stamp duty. Hii anatakiwa alipe mwenye nyumba bahati mbaya tra wanatudai wapangaji inakera na kuumiza sana.
 
Mkuu kupata TIN ni bure ila ili uweze kupata TAX CLEARANCE lazima ulipe ya miazi mitatu hata kama bado hujafungua biashara, maana bila hiyo huwezi kupata leseni ya biashara, kwa hiyo wanakulazimu ulipe kabla hata hujaanza biashara,
 
Mkuu huna biashara na hauwajui vizuri hao watu wa TRA, wakikufungia ujue watakutoza kodi ya tangu umefungua biashara na faini juu, unaeza kuta umefanya biashara hata miezi6 tuu unaambiwa ulipe milioni 3, bora uendenao kibishi tuu ivoivo, siku wakikudaka utajuta, usione makampuni yanafilisiwa ukajua wanapenda ni madhara ya ukwepaji kodi, wee jiulize ya LUGUMI na majumba yote yale hata wakiyauza na hayatoshi kulipa deni alilokwepa kulipa TRA,
 
Weka wazi ni kiasi gani kwa mwaka wamekukadiria, ila navyojua hauanzi kulipa 10% ya mwaka bali robo ya mwaka kama ndivyo wanakuambia ulipe hiyo ni sawa na sh 200000 kwa mwaka sio nyingi, maana kwa kila mwezi ni kama 16000 kama na hiyo inakushinda hiyo sio biashara ndugu, au hauna uelewa wa mahesabu
 
Dada jaribu kutafuta information kwa waelewa wa kodi. Hio ya 10% ni withholding tax kwenya pango, tena kuna additional 1% stamp duty. Hii anatakiwa alipe mwenye nyumba bahati mbaya tra wanatudai wapangaji inakera na kuumiza sana.
Kosa pia ni sisi tunaopewa mkataba na mwenye nyumba haujalipiwa kodi wala hauna mhuri wala sahihi ya mwanasheria
 
Hio 10% ni withholding tax, kapeleka mkataba wa pango wenye thamani ya 500,000/-. Hio ni nje ya makadirio ya kodi ya mauzo kwa mwaka.
 
Hio 10% ni withholding tax, kapeleka mkataba wa pango wenye thamani ya 500,000/-. Hio ni nje ya makadirio ya kodi ya mauzo kwa mwaka.
Asante kunikumbusha mkuu, nilisahau hili,
Na hapo bado hajalipa robo ya mwaka ili apate tax clearance
 
Serekeli yetu kweli masikini na haina wabunifu maana MTU ana kafrem ka saloon ukipiga hesabu items alizonazo hazifiki hata laki 2 lakini mmachinga kapanga vitu barabaran vya mil tano halipi kodi ....
Kosa ni kuwa na mlango
 
acha kupoteza Muda fuga kuku Anza na kuku 300 alafu uje utuambie faida uliipata
 
kama unataka pesa fuga kuku alafu uje hapa?acha story njoo in box
 
Wakuu HV nikienda kuwaambia biashara imenishinda watanielewa kweli au bado watataka niwalipe nimekosa aman, hii nchi yetu jaman inakoendea mbona ....
Hapo cha kufanya ni rahisi tu hata mimi nilishakutana na hali hiyo!!unaandika barua kwa meneja wa tra mkoa kumjulisha kuwa umefunga biashara kutokana na sababu yoyote tu hivyo unamuomba hiyo TIN waisimamishe,utakapo taka kufungua biashara tena utawajulisha,unaandika barua mbili unaenda nazo zote watazigonga mihuri ya kuzipokea moja watakupatia kama kumbukumbu yako!!hiyo ndio ya kuitunza sana uhakikishe imegongwa mhuri wa received!!basi umemaliza ila sasa hujasema hiyo biashara ina muda gani kama kwani hapo kuna installment mbili za kikodi sept na dec!!kwa maelezo zaidi waweza PM,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…