TRA sasa ni Rungu la kuwapiga Wakinzani?

ubongokid

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
2,030
3,908
Kwanza nimpe pole na Pongezi Ndugu Askofu Kakobe kwa kusimamia ukweli;
Pili ni muunge mkono kwamba sio yeye tu mwenye pesa nyingi kuliko serikali bali tupo wengi ambao balance sheet yetu inasoma vizuri kuliko balance sheet ya serikali.

Kitendo Cha mkurugenzi wa TRA kusema anaenda kutafuta kodi kwa Kakobe kwa sababu amesema ukweli ni tusi kubwa kwa Raia wa Jamhuri ya Tanganyika na Kebehi kwa utashi wetu na ni ulimbukeni wa kufunga mwaka.

Kwa taaluma yake na weledi wake nafikiri Mkuu wa TRA ametuthibitishia ukweli kwamba Jamhuri yetu inakaribia kutangaza muflisi.Kwa jinsi walivyopanikishwa na kauli yake na mihemuko ninayoiona pale linapokuja swala linalohusu pesa naona kabisa kila dalili ya bosi wa TRA kushindwa kazi ya kukusanya kodi na badala yake kujiingiza katika propaganda za kisiasa.

Hatua yake hiyo imenifanya nizidi kuwa na shaka na teuzi zinazofanywa za kitaaluma ambazo badala ya kupewa wataalamu wenye weledi wanapewa waganga njaa watu wakujikomba ambao wanadhalilisha taaluma zao kwa ajili ya kipande cha mkate

Ni fedheha kwa msomi mtaalam kukubali kutumika kwa ajili ya kukandamiza watu kwa sababu ya kuwa na kauli zinazokinzana na watawala.

Tanzania ina watu milioni hamsini,haiwezekani katika hao kuwe hakuna wenye mawazo bora zaidi ya watawala.Ni tusi kwetu kufikiri hivyo

Kitendo cha TRA kukubali kuwa Propaganda Machinery kama ambavyo taasisi nyingine nyeti zilivyokubali kutumika ni dalili za kuanza kushindwa kwa propagnda hizo.

Katika hali ya kawaida ni vigumu kuamini kuwa pembeni ya kutudanganya na takwimu za makusanyo nakuchelewa kutupa takwimu halali bado bosi huyu mkubwa anatumia muda wake kujiingiza katika mockery zisizokuwa na maslahi kwa sababu tu anatetea ugali.Historia itamuhukumu.

Nilitarajia sasa hivi angekuwa anapitia kwa karibu mfumo wa kodi ili kuweza kufahamu namna bora ya kukusanya kodi bila kufanya ulipaji kodi kuwa mzigo kwa wananchi.

Badala ya kutumia muda wake kuto elimu na kuchukua maoni ya wadau juu ya viwango vikubwa vya kodi anatumia muda wake kurushiana vijembe na Kiongozi wa dini.

Yumkini anatamani hata angeweza kukusanya kodi toka katika sadaka ili aboreshe makusanyo yake.Huyu mtu aweza kuwa ni kichekesho kwa watu wenye hekima

Any way,Kakobe aliwaambia kama mnashida ya pesa za kutoa huduma,mumuambie tu atawasaidia kwa hiyo ushauri wangu kwenu ni huu:

Utakapotuma kwanza vijana wako waambie wamuombe tu mzee Kakobe anaweza akawagawieni vijisenti vya kusukuma njaanuary maana najua njaanuary itakuwa ngumu sana.

Nawatakia kila la heri katika ukusanyaji wa mapato ya serikali

Wasalaam

PBK
 
Hii nchi imekuwa ya kijinga sana,na watawala wameshatuona sisi hamnazo.
Twende tu
Tusitukane,tutoe mawazo mbadala au tuboreshe kauli ya big boss wa kodi.
Pamoja na kauli yake ya kuwa na mkwanja zaidi ya serikali,alizungumza mengi ambayo wengi hatukubaliani nayo,hivyo basi ni wakati muafaka kama Mamlaka zingine zingejitokeza kama TRA kujiridhisha kwa aliyeyasema...na endepo hawataridhika basi apelekwe Mahakamani kwa kutoa data/statements za uwongo.
 
Back
Top Bottom