TRA ni wakusanya kodi au watoa adhabu?

TRA ni wakusanya kodi au watoa adhabu?

Shedafa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2008
Posts
802
Reaction score
175
Kwa haya yanayoendelea kwenye zoezi la uhakiki inaonyesha TRA wanajiondoa kwenye kazi yao ya kukusanya kodi na kuhamia kwenye kutoa adhabu kwa Watanzania. Nipo uwanja wa Taifa, watu wameacha shughuli za kujitafutia riziki na inasemekana itakuwa siku nzima. Pia haina uhakika kama leo tutafanikiwa, wanasema inaweza kulala hadi kesho.

Hii ni adhabu!
 
Suala zima la uhakiki wa Tin ni adhabu, aidha hawajajipanga au hawaheshimu kazi za wengime.
 
Najiuliza kwa sauti, hivi wangepata hasara gani kama wangeweka watumishi wa kutosha pale uwanja wa taifa na kuweka muda.

Mfano, kuhakiki Tin ni kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 5.

Kwa mara ya 2 leo nimeshindwa kuhakiki, nimekaa naona muda unakwenda tu hata kundi la kwanza lililoingia saa 2 asubuhi mpaka saa 4 na nusu lililuwa halijatoka.

Kwani hii ni dharula?
Si wana idadi ya watu waliotegemea kuwahudumia?

Wakati serekali ikisisitiza watu kufanya kazi wao wanashiriki kurudisha moyo huo. Mfano kati ya wanaotaka kuhakiki na madaktari wapo, ukimuweka kutwa nzima kwa jambo lisilo la dharula anahudumia wagonjwa saa ngapi?

Hebu wakubwa tembeleeni kwenye hivi vituo muone kama kweli tutafika kwa hali hii!
 
Back
Top Bottom