TRA ni vipi wamevuka kiwango cha makusanyo 106% wakati kodi kibao bado hazijakusanywa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA ni vipi wamevuka kiwango cha makusanyo 106% wakati kodi kibao bado hazijakusanywa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sobangeja, Jun 17, 2012.

 1. S

  Sobangeja Senior Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Akijigamba waziri wa fedha na uchumi alidai mamlaka ya mapato Tanzania TRA wamekusanya kodi ya zaidi ya asilimia 106%.Je, kiasi hicho cha kodi kilichokusanywa kinalinganishwa dhidi ya kiasi kipi? Wakati tunaambiwa TRA imeshindwa kukusanya kodi toka makampuni ya madini kwa takribani bilioni moja kila mwezi.Makampuni ya simu yaliyoko Tanzania yamelipa kodi ya trilioni 1.7 kwa wateja milioni 15 wakati Rwanda yenye wateja 4.4 milioni imekusanya kodi inayozidi trilioni 32,Je wizi huu TRA wameubaliki na kukubaliana nao?Mbunge wa jiji moja gari lake halijalipiwa kodi ya mapato kwa zaidi ya mwaka mmoja.Je watu wa aini hii wapo wangapi na ni kiasi gani hakijakusanywa? Nionavyo mimi hicho kiasi walichokusanya hakilingani na kiasi halisi walichopaswa kukusanywa.Hii ni kiini macho kuonesha serikali hii inafanya kazi kumbe hakuna lolote.Karibuni wa JF wenye data za kina tuchangie juu ya hili la kukusanya kodi 106% wakati kodi kibao bado hazijakusanywa.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Marcus mwanaharakati amelitolea ufafanuzi hilo swala,amesema kwamba malengo waliyoweka TRA ni mabovu ndio maana wameyavuka kwa 105%,aliendelea kusema hayo malengo yao ni wamekusanya kodi walizokimbizana na wamachinga,mama ntilie,wavuta sigara na wanywa pombe,kodi kubwakubwa za madini na makampuni ya cm ni zero! Alimnukuu nyerere(jkn) kwamba serikali ya tz ni legelege kwani haikusanyi kodi(hasa za maana,migodi na cm) inabaki kukimbizana na wafanyabiashara ndogondogo(wamachinga,waokota makopo etc)
   
 3. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu TRA haya malengo wanajipangia wenyewe hivyo ni rahisi sana kujipangia lengo dogo ambalo wataweza kulivuka. Ni sawa na nijipangie lengo la kulima robo eka kwa mwaka, nifanikiwe, halafu nianze kujisifia- huo ni upuuzi mtupu!! Imefika mahali sasa malengo yao pamoja na taasisi na mashirika mengine ya umma yapangwe na taasisi tofauti ili watu wawezo kufanya kazi wanazolipwa nazo
   
Loading...