kerubi afunikaye
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 1,183
- 1,061
Wadau wenzangu humu Jf naomba mnielimishe labda mimi sijaelewa.Nimekwenda kulipia road licence ya gari yangu TRA.
Kufika pale nikapewa figure kubwa mno.Nauliza naambiwa ni road licence, penalty ya miezi miwili na makato ya fire extinguisher.
Nikawaomba hiyo fire extinguisher wakasema hawatoi.Nikawauliza kama wao hawatoi niifuate wapi, wakasema nikanunue madukani zimejaa tele.
Nikawauliza kwa nini sasa wanatoza hii kitu kwenye road licence wakaniambia nikaiulize serikali, wao ni watekelezaji tu.
Sasa kabla sijafika ikulu kwa serikali, nimeonelea nije humu jf kwenu watanzania wenzangu niwaulize kuhusu hii kitu, hivi hii ni haki jamani? Ulipie kitu usichopewa halafu bado huko barabarani sheria inakubana uwe nacho, na ukienda dukani unakinunua elfu 12, 15 huku TRA wameshakulipisha 30000 bila kukupa? Sasa hizi elfu 30 za nini? Wengine tayari tulishakuwa nazo hizi kitu tumenunua huko previously, sasa kwa nini nazilipia? Hebu naomba elimu kwa mlipa kodi hapa.