TRA na kodi ya majengo ulaji mtupu

Pole sana.
Na hiyo ni 2016/2017, tarehe 17/07/ 2017 inakuja ya mwaka 2017/2018
 
Pole sana.
Na hiyo ni 2016/2017, tarehe 17/07/ 2017 inakuja ya mwaka 2017/2018
Hivi jama utaratibu ukoje?
Unaanzia kwa mtendaji wa mtaa au unaenda moja kwa moja tra au makadirio yanapatikanaje?
Wengine hatujalifanya hili zoezi na tunahofu yasijekuwa ya vituo vya mafuta!!
 
Unaanzia kwa mtendaji/ serikali ya mtaa utapewa fomu nakuijaza, uta ambatanisha na copy ya kitambulisho chako, itapigwa muhuri hapo serikali ya mtaa kisha utaenda Tra kulipia..
 
Kwanini hukufuatilia? Lazima risiti ifanane na bei waliyoiandika kwenye hiyo barua yao. Inawezekana pia mchapaji alicopy barua ya mtu mwingine.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
....wewe unachotuambia siyo kweli kabisa!! TRA hawapokei any cash, unapewa bili unaenda kulipa bank au Max malipo then unarudi tena TRA kupeleka hiyo pay slip.
 
Labda Hiyo nyingine itakuwa kodi ya malipo ya kodi, hapo ungegoma kuondoka mpaka upate chenji kamli, naona umeamua kuweka jina na TIN yako wazi kupitia hiyo risiti, hizo ni "personal data", mtu anaweza kukudhuru kupitia taarifa zako
haya mdhuru sasa kama ni rahisi hivyo

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Lakini hii kodi INA vituko vingi. Mtaa mmoja wananchi wenye nyumba za kufanana wanalipa kodi tofauti.
Binafsi nimeandikiwa thamani ya nyumba iliyopo chanika kuwa ni Tshs. 44M na kodi ni Tsh 67 elfu
Lakini kuna wengine hakuna makadirio na wanalipa tsh 15,000.
Nyumba yangu ni ndogo na wala haina hata thamani husika kwa kuwa ni vyumba vitatu hata floor haijasakafiwa
Sijafahamu ukadiriaji ulikuwa unaangskia kitu gani
Kuna tatizo kubwa sana kwenye ulipaji wa kodi hii

Post sent using JamiiForums mobile app
 
haya mdhuru sasa kama ni rahisi hivyo

Post sent using JamiiForums mobile app
Sina nia ya kumdhuru ndio maana nimetoa angalizo asijisahau kuachiw hizo taarifa, tatizo Watanzania wengi tunapenda ujuaji na ligi zisizo na maana, moja ya sifa za mtandao huu ni kuwapatia watu fursa ya kutokujulikana utambulisho wako (anonymity), kuna watu humu wameshatafutwa sana mpaka muanzilishi wa JF mwenyewe aliwekwa ndani kwa kugoma kutaja taarifa binafsi "Personal Data" za huyo aliyekuwa anawindwa.

Inawezekana huyo mtoa maada asiwe yeye anyewindwa lakini akawa anajuana na yule anayewindwa na kuna watu humu kazi yao ni kufuatilia mazungumzo ya wengine (wapelelezi) kutokana na sheria mbovu ya mitandao ambayo inaipa serikali nguvu ya kubana uhuru wa maoni pale itakapojisikia, hivyo kwa kuweka jina lake tu walioko hapa kazini wanaweza kumpata na hata kumbana atoe taarifa zaidi. Hawa watu wana mbinu nyingi sana na ID feki na imewahi kuongelewa humu siku za nyuma, ukiweka jina lako na TIN ni kama umempa fisi mfupa, watakudaka tu.

Zamani mtandao yani internet ulikuwa ukichukuliwa kama ni kitu tofauti na maisha halisi lakini hivi sasa internet ni maisha halisi na chochote unachokifanya mtandaoni kina madhara ama manufaa kwako moja kwa moja.
 
Hivi jama utaratibu ukoje?
Unaanzia kwa mtendaji wa mtaa au unaenda moja kwa moja tra au makadirio yanapatikanaje?
Wengine hatujalifanya hili zoezi na tunahofu yasijekuwa ya vituo vya mafuta!!
Mkuu kwanza unaenda kwa mtendaji kuna fomu utapewa utaijaza kisha utaenda TRA huko ndo utakapo ambiwa ulipe kiasi gani
 
In a nutshell we ni Boya.. kwa hiyo hiyo receipt uliisoma ukiwa umeshafika home?
 
Ukitaka kumficha mbongo weka taarifa kwenye maandishi
Vumilia mdau si ww hata first class member tz kwa hilo nao ni waduanzi

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Malalamiko kama haya siungeyafikisha live kwa management kwa maandishi?
 
Kumbe wanatoa mpaka Risiti ?
Jamani tusaidiane wengine tumebakia na kijikaratasi cha kulipia benki tu!
 
Kwani usipolipa hiyo Kodi wanakufanya nini..wanakuja kukufukuza kwako????yaani mimi nilipe Kodi alafu anatokea mjinga mmoja anayejiona kuwa pesa za nchi hii zote ni zake na anaweza kuzifanyia chochote?????sifanyi ujinga huo
 
Duuh pole , ingekuwa mm ningeanzisha tibwli la asha ngedele balaa, et tinasema rais wawanyonge hadi nyumba zetu za tembe tunazilipia kodi, kwA hiyo nyumba nimeijenga mwenyewe sina haki ya kuish kama sina hiyo kodi kaaah balaa.

Kwel hapa kazi tuu
 
Mkuu haihitaji elimu hata ya darasa la nne kujua kwamba umeingizwa mjini, malipo yoyote utakayoyafanya popote pale kama hayaonekani kwa utimilifu kwa kadri ya ulivyotoa basi ujue ziada ni chakula cha watu. Pili mambo ya ukadiriaji wa jengo Mkulu alishayatolea tamko kwamba hayapo na kwamba kodi ya jengo ni 15,000 bila kujali thamani ya jengo.

Mimi binafsi nilikwenda ofisi za TRA na kujaza fomu ambayo ni tofauti kidogo na zile za mwanzo kwa vipengele viwili; kwanza fomu ile haikuwa na kipengele cha kukulazimisha upate signature ya serikali ya mtaa (hapa nawapongeza kwani imerahisishwa ikizingatiwa serikali ya mtaa nako kulikuwa na nyomi),pili haikuwa na kipengele kinachotaka ukadirie jengo. Hatimaye nikalipa Tsh 15000 na kupata risiti yenye kuonesha kiasi hicho. WEWE ULIKUTANA NA OPPORTUNIST.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…