Kwanza, hongera kwa kuwa na familia Kariakoo. Si jambo dogo, lazima uwe mpiganaji.
Pili, za kuambiwa changanya na zako. Ni kwamba kwa sasa wanaanda orodha ya stoo za kuhifadhia mizigo ili wawaandalie utaratibu mzuri wa kuwatoza ushuru. TRA kazi yao ni kukusanya mapato na kutunza kumbukumbu za Walipa kodi. Sasa taarifa za stoo za nini?
Tatu, kulipa kodi ni wajibu. Wapo wafanyabishara wengi wenye stoo wanamaliza biashara huko. Wanaikosesha serikali mapato. Lazima wafanye namna wapate. Tulipe kodi kwa Maendeleo ya Taifa.
Nne, wewe nenda na upepo. Ukiona wenzako baadhi wamefungua nawe fungua. Ukiona kimya, nawe kaa pembeni subiri mgomo uishe. Muda mwingine kuwa wamoja ni jambo la maana hata kama jambo linalofanyika lina ualakini. Kufanya biashara huku wenzako wamekaa tuli, utajijengea chuki.
Tano, nakutakia kila la kheri.