TRA mnakosa mapato kuweni wabunifu

Magari ya kukodisha

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
412
695
Wakuu habari:
Kwanza niseme kwa dhati kabisa toka moyoni napenda kumpongeza rais wetu wa jamhuri ya muungano kwani hadi sasa ameonyesha nia ya dhati kulinasua taifa letu kutoka kwenye wimbi kubwa la umaskin

Rais ameonyesha nia ya dhati kuboresha maisha yetu kutokana na ukusanyaji kodi

Hapo kwenye kodi ndio penye mzizi wa thread hi.
Ushauri wangu Kama itawezekana rais wetu aongee naTRA waongeze ubunifu kwenye kukusanya Kodi mfano: Marekani unaruhusiwa kuwa na plate number yenye jina lako kwa gharama za dola 10 tu mwaka mzima

Marekani inajumla ya magari 268million
Tanzania inajumla ya magari 380000 kwa takwim za mwaka 2015

Sasa hapo Tra inapaswa kujua siku hizi vijana wengi ndio wanaongoza kununua magari na vijana hawa kwakuwa ndio nguvu kazi ya taifa kwanini TRA isibuni vitu mbalimbali vitakavyovutia makundi haya Kisha itakusanya Kodi yake ,

Tanzania ukitaka gari yako iwe na plate namba yenye jina lako ni milion kumi idadi ya magari yaliyopo Tanzania ni ndogo mnooo

Wenzetu Marekani ukitaka kusajili plate number yenye jina lako ni 20000 za kitanzania

Mimi najiuliza TRA kwanini vitu vingine isibuni toka kwa mataifa mengine ili ijikusanyie kodi katika mfumo ambao raia watakuwa wanafurahia maisha.

Vitu vingine vinashangaza sana haswa ukiangalia gharama za usajili wa plate number zenye jina binafsi unaona kabisa TRA hawako serious kutengeneza mazingira ya kukusanya kodi...
 
Sasa ukinunua gari ndio inageuka kuwa nguvu kazi au mimi ndio sijaelwa uhusiano kati ya kodi na nguvu kazi?
 
Rudi kasome upya bandiko ndg.
Ila kwa kukusaidia amesema vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa na hao ndiyo wenye miliki ya magari kwa wingi.
Sasa ukinunua gari ndio inageuka kuwa nguvu kazi au mimi ndio sijaelwa uhusiano kati ya kodi na nguvu kazi?
 
Wewe ndio usaidiwe, kuwa na private number ni want sio need

Nguvu kazi inahusianaje na kumiliki gari ukaweka private number?
Rudi kasome upya bandiko ndg.
Ila kwa kukusaidia amesema vijana ndiyo nguvu kazi ya Taifa na hao ndiyo wenye miliki ya magari kwa wingi.
 
Mbona hiyo ya plate number yenye jina ipo bongo na wanalipia TRA mahela chungu nzima siyo hiyo 20,000/ yako ulosema
 
The late Professor Maji marefu mbunge alifanya hivyo, Dokta Mwaka alifanya hivyo baadae akaacha, na wengine wengi
 
Ndiyo maana Lowasa alikazania issue ya elimu, Elimu, Elimu alijua watu kama wewe hamkosekani, Pole.
Wewe ndio usaidiwe, kuwa na private number ni want sio need

Nguvu kazi inahusianaje na kumiliki gari ukaweka private number?
 
Back
Top Bottom