Wenye magari namba (A) tuwe waungwana tuyatoe barabarani ili TRA warudi kusajili (A) tena itakapo jaa namba D

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Katika utaratibu wa maisha Africa inabidi tujifunze kujiwekea kikomo!

Ili tuendane na ulimwengu lazima tujifunze kubadilika!

Nikimnukuu bwana Newton mwanasayansi msomi aliwahi kusema kwamba (Kila kitu hubaki kilivyo au kwenye mwendo hadi pale nguvu hasi itakapotumika)

Hii inamaanisha kwamba afrika tutaendelea kuwa hivi hivi hadi pale nguvu nyingine itaamua vinginevyo!

Afrika huwa hatuna mda kabisa wa kuzingatia uchakavu (expire date)!

Hatuzingatii uchakavu kuanzia vyakula, mapenzi na vitu vingine yabisi hadi pale tunakumbana na madhara! (Sitachimba sana huku)

Tukirudi kwenye gari na vyombo vya moto!
Huko yanapotengenezwa magari mfano Japan na kwingineko!

Ziko taratibu walizojikwekea kwamba gari ikifikia kiwango flani cha matumizi iondolewe barabarani!

Na ndiyo maana japani ukiwa na hata laki nane unapata gari kari!

Lakini likifika afrika huwa ni Jipya!

Sasa basi, magari yanayoingia inchini husajiliwa na mamlaka ya TRA kwa alphabet kimahesabu ya probability/possibility!

Magari yaliyotumiwa huko inje miaka hiyo, yakafika Tanzania na kusajiliwa namba TZ na baadae kuhamia usajili mpya wa namba (A) hakika yatakuwa yamezeeka sana!

Kama kweli tunajali afya za watu hayo magari yangeondolewa barabari! TRA wasihamie namba E bali waangalie namna ya kuondoa (A) ili waanze upya!

Tunajaza sever za TRA pasipo sababu ya msingi na minamba kibao!

Utafiti unaonesha kama TRA itahamia namba (E) itachukua karibu miaka 8-10 kufikia kujaa!

Rai yangu kwa serikali, kama ilivyofanya kurudia usajili wa laini za simu!
Basi isione tabu kufuta usajili wa magari namba (A)
Serikali ni afadhali ipunguze ushuru wa kuagiza magari Japan lakini ifute usajili wa magari namba (A) ili kubalance life cycle ya magari Tanzania! Iwe (A to D)

Na kwa Yale namba (A) yatayobainika yanaubora wa kiwango cha kubaki, walipie gharama annually na wabadilishwe rangi ya plate number, isomeke namba (A) lakini plate nyekundu (namba maalum)

Mkishindwa hilo, wekeni hata utaratibu wa kila gari kuwa na umri wake wa kutembea!

Nasema hivi kwasababu zipo gari hapa bongo hata akiiona mjapani atakataa kuwa hakuitengeneza yeye!

Yaani gari Kuanzia injini imebadilishwa, gearbox nyingine, kila kitu kimebadilishwa!

Pia Hii inachangia hadi wizi wa spea kuongezeka!

Sioni sababu ya kuhamia namba (E) na kuiacha (A) ikiteketeza dunia kwa uchakavu!
 
Sasa dmkali uwe specific bwana magari gani.
images (37).jpeg
images (38).jpeg
images (39).jpeg
 
Kuna gari limetoka Japan namba D ni bovu vibaya sana na limetumika kuliko namba A

Gari ulinunua lina kilomita ngapi?

Gari namba D lina kilomita 170,000 na namba A lina kilomita 165,000

A, B, c or D are just numbers

Ukitaka gari lako liwe na namba A lipia million tano TRA utapata

Nenda TRA lipia Milioni tano watakupa special numbers inayoanzia A

Sent from my INE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Nguo pia Zina expiry date ni musimu mfano msimu wa baridi ukiisha unapoanza msimu wa joto unatakiwa kutupa wewe mleta mada nguo zako vipi?

Njia nyingine kujua hutakiwi kuendelea kuvaa hiyo nguo Ni je umeifua nguo Mara ngapi ukiifua Mara 20 au ina miezi mitano ya kuwa nayo kizungu shelf life hata Kama umeifua Mara 10 tu unatakiwa uitupe ndio maana huweko kitu kinaitwa sale unanunua nguo iliyokaa muda mrefu kwenye shelf wewe mwenzetu vipi? Kanguo tu ka ndani umekafua au uko nako muda gani Sasa? na bado umekakomalia tu

Ukiondoa mitumba asilimia kubwa ya wananchi watatembea uchi
 
Unaweza onea wivu kitu kibovu
Kibovu vipi wakati hata ukipeleka kwa vehicle inpector traffic anathibitisha kuwa gari Ni nzima? Hata ukipima kwa computer gari inaonekana nzima?

Nchi zinazotengeneza magari au Nchi za viwanda zilizoendelea zinazotegemea viwanda wenye viwanda ndio wanaoimiliki serikali ndio waamuzi wa nini kifanyike kwenye nchi

Kuongeza mauzo ya bidhaa zao Kama magari nk ndio Waka set expiry date ili utake usitake ukanunue lingine pia Ni njia yao ya kuongeza faida mfano Bei halisi ya kutengeneza gari kiwandani aina ya Prado kwao ni milioni mbili. Wanamuuzia mjapani mwenzao milioni tano mfano anatumia Lina expire baada ya miaka mitatu mfano analiuza Tanzania kwa milioni 48.

Huyo mjapani mwenyewe atapenda Sana kununua magari , kutumia na kuyauza!!! Maana anakuta anapata faida kwenye huo mchezo.Kiwanda kinapata faida na mjapani wa kawaida anapata faida.

Sasa Sisi huku ukinunua Prado lako ukilitumia ukitaka kuliuza Tena kwa faida kupata mnunuzi hata ukitaka kuuza kwa nusu bei hasara kumpata mnunuzi itahitaji ukaombewe na kukanyaga mafuta Kwa Mwamposya sio rahisi kupata mteja.Ndio maana serikali kukuhurumia hawaweki kipindi Cha expiry date ya kigari chako Koko
 
Una hoja nzito na yenye mashiko lakini 'wenye magari yao na pesa zao' hawatazizingatia zote. Watakimbilia kushambulia hoja ya '....yaondolewe'
 
Umedhihirisha mwenyewe NYIE ndo watu ambao mkipewa madaraka akili zenu hazipishan na mleta tozo

Ebu fikria Tanzania hatuzalishi hata baiskel alafu et muweke expired ya gari, ? Umetumia akili Gani ww mleta nada?

Nadhan kitakacho jaZa sever za tra ni hayo makolokolo uliyotaja mara number plate nyekundu special, mara uangalizi maalumu TANZANIA yetu bado ipo analogy huo uangalizi maalumu inakuaje?

Polis traffic amini hawajui hata aina za magari Wala vipuri vyake je watakaguaje au ndo

UMETUMWA KUMUHUJUMU MAMA KAMA BWANA YULE, ALIE OA BONGO MOVIE

SIT DOWN AND THINK AGAIN AND AGAIN
 
Kibovu vipi wakati hata ukipeleka kwa vehicle inpector traffic anathibitisha kuwa gari Ni nzima? Hata ukipima kwa computer gari inaonekana nzima?

Nchi zinazotengeneza magari au Nchi za viwanda zilizoendelea zinazotegemea viwanda wenye viwanda ndio wanaoimiliki serikali ndio waamuzi wa nini kifanyike kwenye nchi....
Umemaliza mchezo; tatizo linaanzia kwa anayepanga Prado kununuliwa 48m.
 
Kibovu vipi wakati hata ukipeleka kwa vehicle inpector traffic anathibitisha kuwa gari Ni nzima? Hata ukipima kwa computer gari inaonekana nzima?

Nchi zinazotengeneza magari au Nchi za viwanda zilizoendelea zinazotegemea viwanda wenye viwanda ndio wanaoimiliki serikali ndio waamuzi wa nini kifanyike kwenye nchi..
Uchakavu unapimwa kwa vitu vingi! Na sioni sababu ya kupaniki kama gari litagundulika linafaa, litabandikwa plate nyekundu ili kutofautisha na (A) mpya!

Lengo pia ni kufunya clean sheet namba A!

Tunahitaji kama inchi kuwa na mkakati wa sheria ya uchakavu, mazingira na usalama wa watu
 
Umedhihirisha mwenyewe NYIE ndo watu ambao mkipewa madaraka akili zenu hazipishan na mleta tozo

Ebu fikria Tanzania hatuzalishi hata baiskel alafu et muweke expired ya gari, ? Umetumia akili Gani ww mleta nada?....
Mleta mada atakuwa afisa wa serikali entitled kigari kipya Cha serikali au wake entitled kukopeshwa vigari vipya na serikali .Hai huwa Ni wale akina maskini akipata ma Nani hii hulia mbwata!

Anaiona dunia yoote yake na wengi huwa wale waliezaliwa familia maskini Sana halafu wakafika hizo level za uafisa serikalini .Huwa jeuri na washamba na wajinga jinga fulani hivi .

Wangekuwa sekta binafsi asingeandika hii hoja.Hoja Kama hi inaletwa na malofa wa porini waliopewa vimadaraka serikalini

Ukisoma between the lines unajua kabisa mwandishi anatokea familia maskini Ila kwa Sasa ana ka position koko
 
Uchakavu unapimwa kwa vitu vingi! Na sioni sababu ya kupaniki kama gari litagundulika linafaa, litabandikwa plate nyekundu ili kutofautisha na (A) mpya...
Kwani ikibaki na namba A hiyo hiyo wakati bodi nk vimeboreka Kuna shida gani? Gari inachekiwa na vehicle inspector kila mwaka ubora wake shida nini? Unataka tozo za kubadili namba? Watu waache shughuli zao waanze safari za TRA?
 
Back
Top Bottom