TRA mapato

AyM

Member
Dec 7, 2016
17
22
Nataka kucheki kwa simu kama natakiwa kulipia kiasi gani mapato TRA, gari. Msaada tafadhali namba zao wamebadlisha au ni zile zile 15341 ? Nimejaribu kutuma hapo lakini msg haiendi. Nimebadilisha simu lakini bado haiendi.
 
Kwanza unapaswa uwe na salio la kawaida (wanakata kama tsh. 200 kwa sms) na sio sms za kifurushi...

1. Andika kadiria acha nafasi namba gari (t123aab) tuma kwenda 15341. Hapo utapa kiasi unachodaiwa

2. Andika neno sajili acha nafasi namba ya gari (t123aab) kisha tuma kwenda namba 15341. Hapa utapata makadirio yako.

3. Ingia kwenye Menu ya Mpesa,tigopesa au airtel money.. chagua namba 4. (Lipa bill yako) alafu chagua majina ya kampuni then TRA alafu chagua motor vehicle/ada za mwaka za magari. Baada ya hapo utaambiwa ingiza namba ya kumbumbu.. utaingiza namba uliyoipata baada ya kuandika sajili (namba 2).. namba hyo inakuwa na tarakimu nane.

4. Ingiza kiasi unachidaiwa, ulichopatiwa baada ya kuandika kadiria (namba 1).

Baada ya hapo utapatiwa sms kwamba tembelea ofisi za TRA kuchukua sticker... mara upatapo sms unaweza kwenda ofisi za TRA au sms ikichelewa unaweza tembelea TRA kujua kama malipo yako yamepokelewa ili waprint sticker.
 
Back
Top Bottom