TRA Lindi yagawa tani 133 za sukari iliyoingizwa kimagendo

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,951
29,534
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imegawa Sukari yote ya Magendo Mifuko 5,319 yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi Milioni 373.5 kwa Taasisi mbali mbali Mkoani Lindi baada ya kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kuwa ni Salama kwa matumizi.

Sukari hiyo ilikamatwa mwezi Februari mwaka huu katika bandari ya Lindi ndani ya meli ya MV Hassanat ikiingizwa kinyume cha Sheria ikitokea nchini Brazil kupitia Zanzibar.

Sukari hiyo ilipaswa kulipiwa Kodi zaidi ya shilingi Milioni 246.

Sukari hiyo imegawiwa kwa taasisi 31 mkoani humo baada ya TFDA kuthibitisha kuwa sukari iko salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa sukari hiyo Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema baada ya kukamatwa kwa bidhaa hizo TRA kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali ikiwemo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, iliamriwa sukari hiyo kuigawa kwa watu wenye uhitaji katika mkoa huo zikiwemo taasisi za elimu, Afya, kambi za wazee na Jeshi la magereza.

Chanzo: TBC
 
Iuzwe kwa bei elekezi
Itagawanywa bure mkuu...
Kwa sbb walikurupuka kuzuia sukari kuingia nnchini kumbuka makampun mengine yalikuwa na mikataba ya mwaka or miez sita . Mengine yalikuwa yameshaagiza wangetakiwa wapewe muda kama miez 6 na kuendelea kumbuka mwenye kampun ameajir watanzania na anawalipa mshahara
Hayo maelezo tutayasikia baadae sasa hivi ni kazi tu
 
Hii ndio tanzania tunayo itaka, magufuli go ,go tanzania go kilamtuu

Ni kweli ndio Tanzania tunayoitaka ya kutenda mambo chap chap sio anaelezwa tatizo leo uamuzi wa tatizo mwakani huo sio uongozi bali ni kupeana muda wa kwenda kuomba rushwa.Ningeshauri serikali haswa raisi Mafufuli hii sukari na mali nyingine zitakazotaifishwa ziuzwe kwa wananchi kwa bei halali na mapato yaingie hazina badala ya kugawa bure.Nchi bado ina shida ya fedha.
 
Mbona mwanzo walisema hiyo sukari ilikuwa imeisha muda wa matumizi?du hatari
 
Ni kweli ndio Tanzania tunayoitaka ya kutenda mambo chap chap sio anaelezwa tatizo leo uamuzi wa tatizo mwakani huo sio uongozi bali ni kupeana muda wa kwenda kuomba rushwa.Ningeshauri serikali haswa raisi Mafufuli hii sukari na mali nyingine zitakazotaifishwa ziuzwe kwa wananchi kwa bei halali na mapato yaingie hazina badala ya kugawa bure.Nchi bado ina shida ya fedha.
Magufuli kipindi cha kampeni alisema hakuna mchakato
 
Hatimaye sukari iliyokamatwa ikiingizwa kimagendo kutoka Brazil imetolewa bure kwa taasisi za umma mkoani lindi.

TUTAFIKA TU!

Source:TBC
Unatukumbusha tu jinsi walivyogawa wale samaki wa magufuli.! Hatimaye ikawa hasara kwa taifa.! Ni wakati muafaka kwa mahakama kudhihirisha uwezo wake wa kulinda haki za binadamu na utawala bora.
 
Back
Top Bottom