taratibu ndugu zangu! tatizo la watanzania hatutaki kutumia channel zilizowekwa kufuatilia tatizo na ikiwezekana kulalamika. binafsi, nilishalalamikia benki mbili, kampuni ya simu na sehemu zingine ambako nilidhani sikutendewa haki. na imani yangu ilikuwa kwamba angalau, kwenye organisation yenye watu mia angalao wapo hata 10 wanaojali, na kweli katika baadhi ya sehemu nilikolalamikia uzembe wa baadhi ya wafanyakazi, walionesha kujali na kushukuru kwa taarifa niliyowapa, ukiacha kampuni ya simu Voda, mpaka leo hawataki hata kujibu, nasikia walipeleka majibu TCRA ambako nako nilipeleka malalamiko yangu, nina mpango wa kufuatilia...ukiacha hilo, ndani ya TRA kuna taratibu kwa wafanyakazi na kuna mkataba kwa wateja ambapo baadhi ya huduma zinatakiwa kutolewa ndani ya siku moja, na ikiwa kuna tatizo, mhusika anapaswa kueleza sababu kwa mteja/mlipakodi na awe na ushahidi wa hilo tatizo, mfano akisema system hai-respond, anapaswa kuwa na ushahidi wa kuripoti tatizo hilo kwa wahusika ikiwa atatakiwa kueleza.kibaya ambacho watanzania wenzangu hawataki ni kulalamika wanapokutana na uzembe wa mfanyakazi mmoja au wawili, mfano unapokwenda pale kaunta unaona kuna foleni, lakini anayetoa huduma afuati utaratibu katika kutoa huduma muuulize kwa nini anafanya hivyo, waweza kumuona mkuu wa kitengo na ikibidim meneja wa idara, haiwezekani wote hao wakawa bogus to that extent.zaidi kuna kadi za mrejesho ambazo wateja wanapewa, mteja anaweza na kwa hakika anapaswa kuijaza na kutumbukiza maoni yake katika masanduku ya maoni, isije ikawa tunalalamika nje, lakini wahusika wanaohitaji kuboresha huduma wanatafuta ushahidi kama huo hawaupati