TRA Kagera yavuka malengo ya Serikali, yakusanya Billioni 16 kwa robo ya mwaka wa fedha 2019-2020

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
Jumla ya shilingi Bilioni 16.18 zimekusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania mkoani Kagera kwa upande wa kodi za forodha na kodi za ndani kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari-Machi 2020 sawa na 110.03% ikiwa lengo lilikuwa ni kukusanya shilingi bilion 14.7

Hayo yamebainishwa na Meneja wa T.R.A mkoani Kagera Bwana Adam Ntoga wakati akizungumza na mwandishi wa kituo hiki akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha Januari –machi mwaka huu.

Bwana Ntoga amesema kuwa kwa kipindi cha Januari –machi 2020 mkoa wa Kagera ulipangiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 14.7 kwa upande wa kodi za forodha na kodi za ndani na wameweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni16.18 na kuvuka lengo walilopewa na serikali .

Aidha ameongeza kuwa ni mafanikio makubwa kwa kipindi hiki kwa kuwa kipindi kilichopita kuanzia mwezi Januari –machi mwaka jana utendaji kazi wao ulikuwa ni 94.5%.

Bwana Ntoga amesema kwa upande wa kodi za ndani mkoa wa Kagera ulipangingiwa kukusanya jumla ya shilingi billion 9.1 na wamefenikiwa kukusanya shilingi bilioni 9.8 sawa na jumla 107.5% ya kwa kodi za ndani Wakati kwa upande forodha mkoa wa Kagera ulipangiwa kukusanya billion 5.6 na walifanikiwa kukusanya billion 6.4 sawa 114.16%

Bwana Ntoga amesema wamefikia mafanikio hayo kutokana na elimu inayoendelea kutolewa kupitia vyombo vya habari mkoani humo pamoja na kuwatumia ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kwa wateja wote ili kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.

Sanjali na hayo amebainisha kuwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali wameweza kufanikiwa kuondoa malimbikizi ya kodi .

Kwa upande mwingine amewapongeza wana kagera kwa ushiriki wao katika shughuli za ulipaji kodi ikiwa nipamoja na kulipa kodi kwa muda muhafaka hasa katika kipindi hiki cha kupambana na virusi vya corona na kuwataka wananchi mkoani humo kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na virusi hivyo zinazo tolewa na serikali.
 
Mnajitangaza kuvuka lengo la makusanyo harafu kila siku mnalilia kukopeshwa na mabeberu
 
Na hapo bado Meli haijaanza kufanya kazi.
Wanatoa kodi kubwa ikiwa na pamoja kuuziwa sukari 3000 wakati huo serikali inaenda kuwekeza dar huku mkoa mzima wa kagera ukiongozwa na bukoba stendi ni ya matope na soko la mabati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mngejua wafanyabiashara walivyonyanyasika robo ya kwanza wasingejisifu,
Biashara bado ni mbaya lakini tulipigiwa simu kila siku ili tukalipe na vitisho vya faini juu.
Hongera yao ila biashara za watu ziko hoi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom