TRA imekusanya zaidi ya trilioni 1 kwa mwezi Januari 2016

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Nimewasikia viongozi wa TRA wakizungumza na waandishi ofisini kwao na waandishi wa habari kuwa tangu mwezi wa kwanza uanze hadi leo wameshavuka malengo kwa kukusanya pesa zaidi ya Trilioni Moja.

Hongera sana kumbe tunaweza kujitegemea tukiamua.
 
Tulio wengi tulitarajia makusanyo ya mapato ya serikali kuwa makubwa miezi ya mwanzo kutokana na kasi aliyoanza nayo Dr.Magufuli. Na hilo ni kutokana na ukweli kwamba wanakusanya madeni/kodi zilizopaswa kulipwa miezi kadhaa nyuma na waliokwepa kulipa kodi ususani hawa ambao Rais mwenyewe aliwapa siku kadhaa walipe wanachostahiki
 
Mimi sioni tija yoyote kwenye makusanyo hayo makubwa ya kodi..

Kwa mfano ma-label technician wote wa MANISPAA ya ILEMELA hawajilipwa pesa zao za kusimamia mtihani wa kidato cha nne mwaka jana...
 
Nimewasikia viongozi wa TRA wakizungumza na waandishi ofisini kwao na waandishi wa habari kuwa tangu mwezi wa kwanza uanze hadi leo wameshavuka malengo kwa kukusanya pesa zaidi ya Trilioni Moja.

Hongera sana kumbe tunaweza kujitegemea tukiamua.

Ila kwa taarifa za ndani zinasema kuna madeni kibao yanaelekea ku-mature mwaka huu na itabidi yaanze kulipwa... kwa hiyo tutakua tunakusanya kodi na kulipa madeni aliyoyaacha mkwere...
 
Msiwasifie sababu mpaka sasa wanakusanya Madeni hakuna chanzo chochote kipya cha mapato walichoanzisha....
 
Ila kwa taarifa za ndani zinasema kuna madeni kibao yanaelekea ku-mature mwaka huu na itabidi yaanze kulipwa... kwa hiyo tutakua tunakusanya kodi na kulipa madeni aliyoyaacha mkwere...
Wamesema wanazielekeza kwenye huduma za jamii kama Afya na Elimu huko ndo wamekupa kipaumbele
 
Mimi sioni tija yoyote kwenye makusanyo hayo makubwa ya kodi..

Kwa mfano ma-label technician wote wa MANISPAA ya ILEMELA hawajilipwa pesa zao za kusimamia mtihani wa kidato cha nne mwaka jana...
Unachanganya habari
 
Nimewasikia viongozi wa TRA wakizungumza na waandishi ofisini kwao na waandishi wa habari kuwa tangu mwezi wa kwanza uanze hadi leo wameshavuka malengo kwa kukusanya pesa zaidi ya Trilioni Moja.

Hongera sana kumbe tunaweza kujitegemea tukiamua.
Waache usanii kwani kuna mwaka wowote TRA walishawahi kusema hawajavuka malengo? Ukiangalia hiyo 1.3 trillion wanayojivunia kukusanya ukiiweka in dollar value ni makusanyo pungufu in dollar terms ukinganisha na kipindi kama hiki last year
 
Mimi sioni tija yoyote kwenye makusanyo hayo makubwa ya kodi..

Kwa mfano ma-label technician wote wa MANISPAA ya ILEMELA hawajilipwa pesa zao za kusimamia mtihani wa kidato cha nne mwaka jana...

label technician ndo nani hao braza
 
Ukusanyaji wa mapato wa Sh 1tr/- kwa mwezi ni kiasi kidogo sana ukizingatia kuwa uchumi wetu unakaribia Sh 8tr/- kwa mwezi. Hii haijafikia hata nusu ya lengo la chini lililowekwa kimataifa la kukusanya 25% ya pato la taifa (GDP). Huu ni utendaji mbovu kuliko katika nchi nyingine yoyote Afrika iliyo na amani katika ukusanyaji mapato. Lakini kwa mfumo wa kiutawala uliopo usiozingatia maslahi mapana ya taifa kama kutokomeza rushwa katika siasa (e.g. ndoa haramu kati ya CCM na wafanyabiashara); kukuza demokrasia na utawala bora; na kuondoa migongano ya kimaslahi kwa viongozi na watendaji wa umma (unaotokana na katiba mbovu), tusitarajie lolote la maana.
 
Waache usanii kwani kuna mwaka wowote TRA walishawahi kusema hawajavuka malengo? Ukiangalia hiyo 1.3 trillion wanayojivunia kukusanya ukiiweka in dollar value ni makusanyo pungufu in dollar terms ukinganisha na kipindi kama hiki last year
Mkuu watz tunapenda namba lakini hatupendi hesabu. Hakuna anayetaka kufanya hiyo hesabu uliyosema hapo. Tunafurahia tu kusikia trillion basi.
 
Back
Top Bottom