TRA ilaumiwe kwa Hali Ngumu ya Maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA ilaumiwe kwa Hali Ngumu ya Maisha

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mozze, Mar 5, 2011.

 1. m

  mozze Senior Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kushindwa kwa serekali kusimamia uwajibikaji kwa umma kumesababisha Ugumu wa maisha nchini kwetu. TRA kama moja ya vyombo muhimu sana katika uchumi wa nchi imekuwa ndio kikwazo kikubwa sana cha maendeleo. Nimefanya uchunuzi wa haraka tu baada ya kukumbana na adha kubwa wakati wa kutoa container langu na kuona kuwa kwa kiasi kikubwa mzizi wa matatizo yote, kama mfumuko wa bei na ukuaji mdogo wa uchumi ni TRA.

  Ninadiriki kusema kwa uhakika kabisa kuwa japo serekali inajisifia kuongeza mapato, kwa kiasi kikubwa mapato hayo yanatokana na unyonyaji wa wananchi wake. Mapato hayo makubwa yanayotumiwa vibaya na viongozi wetu, kama kununua magari ya kifahari, ni matokeo ya unyonyaji wa wananchi kwa sababu TRA wanatoza kodi bila msingi maalumu.

  Ninasema utozaji wa kodi hauna msingi kwa sababu, TRA wanakitengo cha "Valuation" lakini japo nimeshaingiza mali mbalimbali hawajawahi kusema "basis of valuation". Hivyo unakuta leo kitu kilekile unalipishwa kodi nyingi kuliko jana....huu mimi naona ni unyonyaji, na kwa vile kodi wanayokata leo ni kubwa kuliko ya jana basi ni wazi na maisha yataendelea kupanda (inflation).

  Zaidi ya valuation, uzembe mwingine ni kwenye kutoa mzigo, hapa TRA na THA wanahusika. Container langu, kwa mfano, limetumia mwezi mmoja kutoka Japan, lakini baada ya valuation kutoka (pre-assessment) imechukua tena wiki tatu kupata kibali cha kutoa mzigo. Sababu walizokuwa wanatoa ni kuwa wakaguzi wako busy. Ninachoshangaa mtu aliyeajiriwa kukagua mizigo anakuwaje busy? huu ni uzembe ambao bila kujua maumivu yake yanaenda kwa wananchi bila sababu. Kwa mfano moja ya mzigo wangu, Pikipiki, nilitegemea kuuza kwa Tzs.650,000, japo hata value ilipandishwa na TRA, kutokana na hesabu za awali, lakini kutokana na uzembe wa kutoa mzigo itabidi kuuza pikipiki kwa Tzs. 950,000.

  Huu ni mfano rahisi na dhahiri kabisa. Hivyo japo hapa naandika kama malalamiko yangu lakini nimefanya survey ya haraka na nimeuliza wafanyabiashara kadhaa na wote wanakutana na hali hii kila siku, kuanzia kwenye mafuta hadi kwenye vyakula. Mimi nimebahatika kuishi katika nchi iliyoendelea wakati fulani, japokuwa kuna uangalizi wa hali ya juu kwa vitu vinavyoingia, lakini process ya kutoa mzigo bandarini au airport ni haraka sana, ndani ya 2days mzigo umetoka...na matokeo yake wameweza kudhibiti sana mfumuko wa bei. Hii ni sababu nchi zilizoendelea mfumuko wa bei ni chini yz 2%, japo kwa kiasi kikubwa wanategemea kuingiza bidhaa na mali ghafi kutoka nchi zetu masikini au china. Sasa kwa nchi kama yetu ambayo uchumi wake unategemea IMPORTATION ni kwa nini kusiwe na usimamizi wa kuhakikisha mizigo inatolewa kwa haraka na ufanisi ili kupunguza ugumu wa maisha?
  Inashangaza sana TRA wanapotoza kodi ya juu kwa vitu muhimu wakati wakiweza kutoza kodi halali inayolingana na thamani ya kitu wataweza kupata kodi zaidi kutokana na faida za hao wafanyabiashara au wazalishaji walioingiza hivyo vitu.

  TRA haina budi kuacha kuwanyonya wananchi kwa kupandisha gharama na bidhaa na uazalishaji, badala yake waongeze ufanisi utakaochochea ukuaji wa uchumu na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa kodi.

  Ni imani yangu kama wananchi tutatoka na kuipigia kelele TRA wajirekebishe na wafanyakazi wake wawe waaminifu basi uchumi wetu utakuwa kwa kiasi kikubwa na maisha yatakuwa nafuu sana.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakika naunga mkono maelezo yako. Hakuna sehemu nzuri kupima inefficiency katika nchi yetu kama TRA mpaka inafika wakati unaapa kwamba sitaagiza mzigo wowote toka nje ya nchi. Wakati mwingine huwa najiuliza kama hiyo ni mbinu ya kutengeneza mazingira ya rushwa na hivyo kunyima mapato ya nchi yetu? Na mkuu wa TRA yuko kimya!
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Badala ya kuingiza toka nje ya nchi, anza kuzalisha humu humu nchini ili uondokana na adha za ushuru na kukuza ajira za WaTZ.
   
Loading...