TRA huu ni zaidi ya unyanyasaji!

TRA huu ni zaidi ya unyanyasaji!

Hapa mkuu nawe umechanganya!! Mi sizungumzii Property tax.Kwani hii hukusanywa na halmashauri husika, japo kwa dar jukumu alikabidhiwa TRA, alichemka.hilo suala lako la PAYE hilo lipo ki sheria, sasa hili la mikataba ya pango inawezekana liko kisheria sasa inakuwaje uniambie mimi kuwa kodi ya mwenye nyumba mnikate mimi eti wao huwa hawakubali!! Hivyo nilipe mimi then nika negotiate naye akikubali kuni refund powa akikataa basi!!! Huoni kuwa kuna tatizo hapo??? Then mnategemea kuongeza tax base kwa mwendo huu!!! Jiulize kwanini TRA walichemka kukusanya hiyo property tax???? Wakawa wanaacha magorofa ya kariakoo wanakimbilia vijumba vya mbagala?? Na inakuwaje mtu akachukue TIN namba wilaya ya mkulanga asikutane na kodi hiyo?! N
io vitu vinavyotakiwa kujibiwa.

Property tax nh kwa kila nyumba na ni kodi ya halmashaurı japo inakusanywa na TRA.Withholding tax nı kwa majengo yanatumika kibıashara kama nyumba za kupanga,frame za bıashara,hotelı,gesti,gereji n.k.Pole,ni ka utaratibu japo kanakera.Ila hawa ma landlord wanakusanya hela nyingi lakn hawataki kabisa kulipa kodi!!
 
Hapo ni sawa,
kodi za majengo zinaangukia katika kipengele cha "Withholding Tax". Hii ni aina ya kodi ambayo hukatwa from "the source". Kwenye fungu hili hata kodi kutokana na mishahara-PAYE zinaangukia humu.

Yaani mlipa hela (Mpangaji au Mwajiri) anamkata kabisa kodi mlipwa hela (Mwenyenyumba au Mfanyakazi) na kuipeleka TRA.

Ukitaka wewe ulipe rent kisha Mwenyenyumba ndio akalipe kodi, vipi waajiri nao wakitaka wawalipe mishahara mizima mizima wafanyakazi wao kisha wao wafanyakazi ndio wakalipe kodi wenyewe?

Tatizo hapa hawatoi elimu ya kutosha kwa wananchi hakuna mtu mwenye akili timamu atakae kataa kulipa kodi. Mi nilitaka kugombana nao nilipo kwenda kulipia kodi ya mapato kwanza nikakuta imepanda kwa 100,% alafu akaniambia nilipe elfu 52000 kwa ajili ya mfanyakazi wangu, yani nikadirio la kila baada ya miezi mitatu. nikahoji inakuwaje Mimi ndio nimlipie wakati anatakiwa kukatwa kwenye mshahara wake akasema huo ndio utaratibu yeye atalipa nawewe kama mwajiri unatakiwa kulipa pia,inaitwa skills development tax. Nikalipa kwa shingo upande lakini roho iliniuma sana, kwakuwa sikujua kama kuna mambo kamahayo.
 
Jana nimekwenda ofisi ya TRA, kwa ajili ya kukata TIN, nafika nakutana na mkadiliaji kodi, ana kadiria kodi ninayotakiwa kuilipa, nakubaliana nayo tena kwa kuvutana kweli, Ngoma ikaja anataka mkataba wa pango, nikampa anasema kuwa eti hiyo kodi ya pango ambayo kwa mwaka ni 1.2 milioni, natakiwa nilipe asilimia 10!!!! Ambayo ni 120,000!! Nikamwambia mimi hiyo pesa nimemlipa mwenye nyumba na yeye ndio anatakiwa kulipa kodi kwenye pesa hiyo sio mimi tena nimlipie?? Anasema eti kwa wenye nyumba imekuwa ngumu kulipa kodi hiyo, hivyo mi ndio nilipe kisha nikamwambie mwenye nyumba anirudishie!! Jamani huu si uhuni, serikali inaogopa kukusanya kodi hiyo toka kwake mi ndio niwakusanyie?? Tumebishana sana nikaona ngoja niondoke zangu kwani naweza leta balaa jingine tena nikampa sifa MGONJA!!! Kweli hii nchi ni shidaaa!!! Wanashindwa kukusanya kodi huko IPTL, Sisi ndio watukamue, haya mambo ndio yanasababisha mtu akwepe kulipa kodi kabisa !!! Hata hicho kidogo kinakosekana kabisa!! Kwani hii sheria imekaaje na mbona huko nyuma haikuwepo??? Yaani mapato amepata mwenye nyumba kodi nilipe mimi jamani!!!! Kisa wenye nyumba huwa hawakubali wanapofuatwa na mamlaka ya kodi!!!

Nimekutana na situation kama hii leo hata saa moja haijaisha. Mimi cjawabishia coz sijui taratibu zikoje.tena nimeambiwa nilipie 132,ooosh kwamba 10% ya kodi ya pango na 1% hata cjui ya kitu gani....
 
Hiyo kodi kama ungelipa ungekua mjinga wa mwaka 2014/2015.

Hakuna kitu kama hicho kama walihitaji hiyo kodi ungewapa mkataba wakafatilia wenyewe hio kodi tena bila ya kukuathiri wewe na mwenye nyumba.

Nchi hii wengi tunashindwa kuelewa haki zetu ni zipi kwakua hawaweki wazi wanatupa zile za kutunyanganya chetu tuu.

Juzi niliwasikia Tra wanasema eti wamefuta kodi za forodha kwakua mashine ziweze kutumika lakini cha ajabu mpaka kesho ukiingiza mzigo unalipishwa kodi hizo za forodha kama kawaida.

Kila mwenye nafasi anakula kwa kamba yake

Embu nishauri cha kufanya mkuu maana na mie ndo nilitaka kwenda kulipa kesho au kesho kutwa
 
Nimekutana na situation kama hii leo hata saa moja haijaisha. Mimi cjawabishia coz sijui taratibu zikoje.tena nimeambiwa nilipie 132,ooosh kwamba 10% ya kodi ya pango na 1% hata cjui ya kitu gani....

Hiyo kitu hipo kwenye sheria ya kodi ya mapato,hiyo ni withholding tax,tatizo ni kwamba tra wako silent kutoa elimu juu ya sheria za kodi lakini ki ukweli kuna kodi nyingi smbazo tunatakiwa kulipa lakini hatuzilipi kwa sababu tra hawazifuatilii na nyingi hatuzijui
 
kama we kilaza wa sheria za kodi tulia usilalamike. ungeuliza kisheria nani anapaswa kuwasilisha hiyo 10% TRA kati yako na mwenyenyumba ili usaidiwe. pambafu. sheria inamtaka mpangaji kabla ya kulipa pango akate hiyo percentage na kuiwasilisha TRA. **** kuna shida ni kwenye sheria wala sio TRA, usiwaonee bure.
 
Na wewe unaweza kuwa mtaalam wa sheria za kodi lkn ukawa kilaza kwny mambo mengine....
Ndo maana jukwaa hili lipo kwa ajili ya kuelimishana kwny mambo mbali mbali
 
Tatizo hapa hawatoi elimu ya kutosha kwa wananchi hakuna mtu mwenye akili timamu atakae kataa kulipa kodi. Mi nilitaka kugombana nao nilipo kwenda kulipia kodi ya mapato kwanza nikakuta imepanda kwa 100,% alafu akaniambia nilipe elfu 52000 kwa ajili ya mfanyakazi wangu, yani nikadirio la kila baada ya miezi mitatu. nikahoji inakuwaje Mimi ndio nimlipie wakati anatakiwa kukatwa kwenye mshahara wake akasema huo ndio utaratibu yeye atalipa nawewe kama mwajiri unatakiwa kulipa pia,inaitwa skills development tax. Nikalipa kwa shingo upande lakini roho iliniuma sana, kwakuwa sikujua kama kuna mambo kamahayo.

hapo kwenye skills levy umeliwa! skills levy au sdl,( kama sheria haijabadilishwa jana), hulipwa na mwajiri mwenye wafanyakazi zaidi ya 4, na ni 4% ya mishahara yao.
 
hapo kwenye skills levy umeliwa! skills levy au sdl,( kama sheria haijabadilishwa jana), hulipwa na mwajiri mwenye wafanyakazi zaidi ya 4, na ni 4% ya mishahara yao.

Ndio, ni SDL. Kuhusu 4% ya mshahara ndio nasikia kwako na nitaifanyia kazi thanks mkuu, wao walisisitiza kwamba ni fix amount ambaya ni 52 elfu kwakila baada ya miezi mitatu.
 
Jana nimekwenda ofisi ya TRA, kwa ajili ya kukata TIN, nafika nakutana na mkadiliaji kodi, ana kadiria kodi ninayotakiwa kuilipa, nakubaliana nayo tena kwa kuvutana kweli, Ngoma ikaja anataka mkataba wa pango, nikampa anasema kuwa eti hiyo kodi ya pango ambayo kwa mwaka ni 1.2 milioni, natakiwa nilipe asilimia 10!!!! Ambayo ni 120,000!! Nikamwambia mimi hiyo pesa nimemlipa mwenye nyumba na yeye ndio anatakiwa kulipa kodi kwenye pesa hiyo sio mimi tena nimlipie?? Anasema eti kwa wenye nyumba imekuwa ngumu kulipa kodi hiyo, hivyo mi ndio nilipe kisha nikamwambie mwenye nyumba anirudishie!! Jamani huu si uhuni, serikali inaogopa kukusanya kodi hiyo toka kwake mi ndio niwakusanyie?? Tumebishana sana nikaona ngoja niondoke zangu kwani naweza leta balaa jingine tena nikampa sifa MGONJA!!! Kweli hii nchi ni shidaaa!!! Wanashindwa kukusanya kodi huko IPTL, Sisi ndio watukamue, haya mambo ndio yanasababisha mtu akwepe kulipa kodi kabisa !!! Hata hicho kidogo kinakosekana kabisa!! Kwani hii sheria imekaaje na mbona huko nyuma haikuwepo??? Yaani mapato amepata mwenye nyumba kodi nilipe mimi jamani!!!! Kisa wenye nyumba huwa hawakubali wanapofuatwa na mamlaka ya kodi!!!
Stimes ukweli ni mbaya sana hapo ungewaambia nyumba ni ya familia. Ila kama hela anapata mwingine alafu kodi unadaiwa ww ni upuuzi.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Ndio utatatibu wanaotumia mkuu, no way you can escape that.
Kama ni utaratibu ni wa hovyo kabisa na wa uonevu! Na TRA ndivyo walivyuo hata hizi kodi za wafanyabiashara wengine wewe unaepata huduma eti ndio uzipeleke. Hivi mishahara miokubwa wanayopata halafu hawataki kuifanyia kazi ni ya nini. Hapana Tumezunduka huo utaratibu si Biblia wala Msahafu ubadilishwe kama ni kweli!
 
Back
Top Bottom