Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,846
- 39,578
Kwa wale wafanyakazi wanajua kwamba kodi wanazotozwa kwa asilimia jinsi zilivyo ngumu na zinauma. Lakini kuna hii kodi tunayotozwa wafanyabishara kwa niaba ya wenye nyumba wetu naona wala siyo sahihi.
Mimi nimepanga kwa mtu nalipa laki mbili kwa mwezi, eti TRA wanataka mimi kwa kila laki mbili ninayolipa kama Pango, nikatwe asilimia kumi. Yaani natakiwa nilipe lakini mbili na elfu arobaini (240,000) kama Kodi ya zuio kwa kodi anayotakiwa kulipa mwenye nyumba wangu kwa mwaka.
Maelezo yao ni kwamba wewe mpangaji uende ukamdai mwenye nyumba wako kodi uliyokatwa na TRA. Swali langu wakati TRA wanajua wapi nilipopanga ni kwa nini wasitengeneze mfumo wa kupata hela yao ya kodi toka kwa mwenye nyumba wangu?
Iweje mimi nilazimishwe kulipa kodi kwa niaba ya mwenye nyumba wangu? Hivi kwa mazingira ya Tanzania ni rahisi kumwambia mwenye nyumba wako akurudishie kodi uliyokatwa na TRA?