TRA hamjawatendea haki INTERNS wenu

CARDLESS

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
7,786
15,726
Jana wakati natoka kazini, nilipata wasaa wa kupitia maeneo yangu ya kujidai TABATA. Kwa bahati nilikutana na kijana mmoja ambaye nilimfahamu kupitia kazi zetu hizi.

Kwa bahati mbaya sana alinijulisha kuwa wamesitishiwa mikataba yao, mbaya zaidi ni kwamba wameambiwa mwisho ni IJUMAA yaani jana na ifikapo J3 hawaruhusiwi kuingia kazini.

Sikuona tatizo kwa vijana wale kumaliza mkataba ila njia iliyotumia kuwapa ujumbe haikuwa sawa, na hasa ukizingatia wangeweza kupewa Barua inayaonesha kuwa kuwa Tar fulani itakuwa mwisho wao.

Inafahamika wazi wale vijana haikuwa ajira lakini kwanini msikae nao na kuwaeleza kwa usahihi? Kwanini muwape stress za ghafla kiasi hiko.

Mamlaka ya Mapato ni taasisi kubwa mno, hivyo utoaji wa taarifa lazima uzingatie pia haki za hao watu.

Mwisho naomba mkae nao muwape hata darasa la namna ya kuishi bila zile kazi, maana nimeona hapa kijana ameshindwa hadi kula chakula.

Nawasilisha.
 
Mkataba ukiisha hupaswi kuonekana eneo la kazi. Ni amri kutii sheria bila shuruti.

Vijana walipewa mkataba wa miaka miwili na kila mwezi walilipwa laki nne na nusu (450,000) per month. Kwa miaka miwili hiyo ni sawa na milioni kumi na laki nane. 10,800,000.

Muulize kijana pesa zote hizo kapeleka wapi? Ilipaswa wakimbizwe kabisa. Tatizo la wabongo hawana shukrani.
 
MKATABA UKIISHA HUPASWI KUONEKANA ENEO LA KAZI. NI AMRI KUTII SHERIA BILA SHURUTI.

VIJANA WALIPEWA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KILA MWEZI WALILIPWA LAKI NNE NA NUSU (450,000) PER MONTH. KWA MIAKA MIWILI HIYO NI SAWA NA MILIONI KUMI NA LAKI NANE. 10,800,000.

MUULIZE KIJANA PESA ZOTE HIZO KAPELEKA WAPI? ILIPASWA WAKIMBIZWE KABISA. TATIZO LA WABONGO HAWANA SHUKRANI.
Hizo Ela kwani zilikua zinaingia zote kwenye kibubu mkuu?
 
MKATABA UKIISHA HUPASWI KUONEKANA ENEO LA KAZI. NI AMRI KUTII SHERIA BILA SHURUTI.

VIJANA WALIPEWA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KILA MWEZI WALILIPWA LAKI NNE NA NUSU (450,000) PER MONTH. KWA MIAKA MIWILI HIYO NI SAWA NA MILIONI KUMI NA LAKI NANE. 10,800,000.

MUULIZE KIJANA PESA ZOTE HIZO KAPELEKA WAPI? ILIPASWA WAKIMBIZWE KABISA. TATIZO LA WABONGO HAWANA SHUKRANI.
Motivational speaker bana hio 10.8m utadhani ilikua haina gharama nyingine za Maisha(Kodi,kula,usafiri) etc
 
MKATABA UKIISHA HUPASWI KUONEKANA ENEO LA KAZI. NI AMRI KUTII SHERIA BILA SHURUTI.

VIJANA WALIPEWA MKATABA WA MIAKA MIWILI NA KILA MWEZI WALILIPWA LAKI NNE NA NUSU (450,000) PER MONTH. KWA MIAKA MIWILI HIYO NI SAWA NA MILIONI KUMI NA LAKI NANE. 10,800,000.

MUULIZE KIJANA PESA ZOTE HIZO KAPELEKA WAPI? ILIPASWA WAKIMBIZWE KABISA. TATIZO LA WABONGO HAWANA SHUKRANI.
Huu ni mshahara au ujira mdogo?hii ni sawa na nauli tu kwa kupanda basi 3 za kuungaunga kwa mwezi mmoja.
 
Unaweza kuweka akiba ya shilingi ngapi kwa mwezi kwenye shilingi 450,000?

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
Mimi naweza.kuweka laki 1 na 80.

ibaki 270,000 tu naweza kukata nayo mwezi.

Elfu 9 kwa siku ni hela nzuri tu.

mwaka wa 4 huu sina ajira na Degree yangu halafu kuna mtu alipata hio hela halafu analia!

Kwa kweli Mwenyezi Mungu ana kazi sana katika kuyasikiliza malalamiko ya waja wake
 
Wewe kwenye Kaz zako piga umemaliza miaka mingap? Afu zidisha na kipato chako baada ya hapo onyesha unabeigan cash? Usifanane ka mtoto wa mama anayeish kwao Ina maana hata boxer hanunui au nguo em usituhaibishe inavyoonekana Bado unalelewa wewe
 
Back
Top Bottom