Halafu hawa TRA huwa wananiudhi mimi.
Sijui labda ni umbumbu wangu au vipi,,,,, ila wanakera, wanakera sana tu! AAgh
Labda tujadili haya:-
Mtanzania anayefungua kibanda tu cha kuuza tumaandazi twa watoto,,, kabla hajafungua lazima alipe kodi! jamani kodi hata sijaua biashara italipa ama vipi? Biashara ya mkopo pale pride? Lipa kodi kwanza,,, tax clearance!!! ptuuuuu,,, inanuka hiyo. Aibu hawaoni hawa jamaa hata kidogo,,,, aagh
Upande wa pili anakuja jamaa na mahela yake,,,, nywele zimekaa upande,, sijui mzungu,,, sijui mhindi,,,,anapewa TAX HOLIDAY YA MIAKA MITANO!!!!! five years my friend!!!! UUUUUwi. Eeee habari ndo hiyo bwana. wakimaliza 5years wanabadilisha jina kwenda kwa mtoto, mke au hata mjomba au jina lake la utotoni,,, makampuni yote tunayajua na hawa TRA wanaangalia tu! aah!
Hapa ni sawa na mtoto anataka kwenda shule unamwambia kabla hajaenda shule akupe kitu kidogo kwanza. Kwa nini TRA WASIWAPE WAZAWA WA TANZANIA HATA MWAKA TU WATU WASTUDY BIASHARA KAMA INAGENERATE THEN WALIPE KODI BAADA YA MWAKA TU.
Haya kuna biashara niliona sehemu fulani hapa Tanzania,,,,TRA wanakamata wamama wanaoenda kununua vibidhaa border ambavyo havina hata faida ya shs 10,000. at the same time kuna mfanyabiashara anapitisha container la 40 feet bila kulipia ushuru,,,, oooh my God! na wanajua,, wanamwona ila huyu aliyeenda kununua vijisabuni ili tu ajepushe na balaa anakamatwa na kupelekwa TRA eti wamekamata magendo! Huyu dada yako amesema umalaya basi atafuta tu mia twa mafuta ya taa unamkamata na mara ingine wanalazimishwa hongo ya ngono! Kweli? Halafu mnasema tutafika! Kwa namna hiii? TRA wamelaaniawa na hata maandiko yaliwalaani watoza ushuru!!!!!!!!!!!
Sisemi tusilipe kodi, la hasha, tuwe utaratibu wa kumsaidia Mtanzania ajikomboe na shuruba na ukata unaotukabili.
Narudia sijui kama ni umbumbu wangu ama vipi ,,,,, ila INAKERA MNO!!!!!