TRA, BoT wanalipwa mishahara minene kuliko maprofesa’

Hii ndio bongo viongozi wanaposema wananchi fungeni mikanda wao huwa wanalegeza.

Hata ngazi ya familia baba unaweza kuiambia familia funga mkanda lakini wewe ukapitia baa kula supu au ukiwa kazini ukala chakula tofauti na maagizo ya nyumbani.

Huyu prof bado anamentality za kizamani. Inabidi afanye tena research yake kuhusu mishahara. Kwa miaka hii mishara mikubwa TZ hii haipo tena B0T na TRA!!

HEHEHEH Rejao! Mzima?
Hebu tutonye wenzio, hiyo mishahara imetandaa hadi wapi ukiacha BOT na TRA?

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, amesema sera mbaya za Serikali katika mishahara zimesababisha mgomo wa madaktari.

My take: Inavumishwa wakristo ndio wakosoaji wa serikali Profesa Abdallah Safari kabadili dini?

Nora Damian
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, amesema sera mbaya za Serikali katika mishahara zimesababisha mgomo wa madaktari.

“Mimi ni Profesa wa chuo kikuu lakini mshahara wangu haufiki hata Sh2 milioni lakini huko BoT na TRA kuna watu wa kada za chini kabisa wanalipwa mamilioni ya pesa,”alisema Profesa Safari.

Profesa Safari ambaye alikuwa akizungumza kwenye kampeni maalumu ya chama hicho ijukanayo kama ‘Ondoa CCM Dar’ alisema mgomo wa madaktari unaoendelea sasa ni matokeo ya sera mbovu za mishahara zilizowekwa na Serikali.

Kama mishahara ya maprofesa na madaktari bingwa ni midogo kweli kuna haja TAKUKURU wawachunguze maghari ya kifahari wanayotembelea na mahekalu ya majumba waliyojenga ya kuishi pesa wametoa wapi? pia kuwachunguza mashule makubwa na mahospitali binafsi ya mabilioni pesa wanayomiliki hizo pesa wametoa wapi.TAKUKURU walisilale wahamie kwa madaktari na maprofesa. Pia na TRA wasikae mbali nao inaelekea kuna mapato yanapita nje ya mfumo wa TRA. Hizo pesa walizojengea hayo mahekalu,mahospitali binafsi,mashule na kadhalika ni TAXABLE income wanayotakiwa wa-account for.Kama hizo pesa hawakuzipata kwa njia zinazoeleweka ni vizuri kitengo kinachoshughulikia Pesa HARAMU kiwafuatilie walizitoa wapi.Yawezekana ni pesa chafu.

basi na yeye aende huko BOT au TRA
suala sio kwamba na yeye aende huko, wote ni watumishi wa uma kwann wengine walipwe mishara mikubwa sn wakati huu wengine wa sekta zingine mishara midogo kiasi cha kwamba kukidhi maisha yao shida?. hii ndo inayosababisha migomo za baadhi ya secta na kugharimu maisha ya watanzania maisiki, kumbuka wenye uwezo wataenda fuata huduma popote.

Anafundisha chuo gani huyu profesa? Manake nijuavyo mishahara ya walimu wa UDSM miaka ya hivi karibuni imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana.

Ni kweli mishahara ya walimu chuo vyuo vikuu imeboreshwa sana namshangaa huyu Profesa na mimi pia nauliza yeye anafundisha chuo gani?

Profesa Safari (mjumbe wa kamati kuu chama cha demokrasia na maendeleo). Mpaka hapo nimeshaelewa ni kwa nini kasema hivyo!

suala sio kwamba na yeye aende huko, wote ni watumishi wa uma kwann wengine walipwe mishara mikubwa sn wakati huu wengine wa sekta zingine mishara midogo kiasi cha kwamba kukidhi maisha yao shida?. hii ndo inayosababisha migomo za baadhi ya secta na kugharimu maisha ya watanzania maisiki, kumbuka wenye uwezo wataenda fuata huduma popote.

Nakuunga mkono, watu wengi hawaelewi mada na hoja za watu haraka, kosa la serikali ni kushindwa kuweka utaratibu wa mishahara kwa kada zote unaofanana. hoja hapa ingekuwa marupurupu kutokana na aina ya kazi unayofanya. Na hilo kosa ambalo ni la kibaguzi ndo linawatesa leo. Eti digrii moja ya Udaktari 960,000/- kwa mwezi, digrii hiyo hiyo ya Uhasibu 300,000/-, Sasa hiki ndo kinawatesa, mshahara ungekuwa mmoja harafu tofauti kidogo kwenye marupurupu kama on call allowance ambayo haipo kwa mhasibu n.k.

Na pia ufahamu kusomea Udaktari pale IMTU, Bugando, KCMC, Ifakara na St. John ni zaidi ya 3mil. kwa mwaka wakati huo uhasibu unaosema 3mil. ni ADA ya miaka miwili.Achilia mbali miaka ya kusemea udaktari wenyewe. Tusiwe wanafiki kama mtu anastahili mwache apewe na kama na wewe unataka bado hujachelewa TCU bado hata hawajafungua pazia unaweza kwenda chuo chochote kati ya hivyo vilivyotajwa hapo juu, hii ni kama kichwa chako kinauwezo....heeheee!

Anafundisha chuo gani huyu profesa? Manake nijuavyo mishahara ya walimu wa UDSM miaka ya hivi karibuni imeboreshwa kwa kiasi kikubwa sana.

Una uhakika na hicho unachoongea au ni redio mestini?Kama unajua mishahara ya wahadhiri imeboreshwa ebu tujuze kwa kiasi gani?Unazijua posho zinazolipwa na viongozi wastaafu wa ngazi za juu hapa nchini? If you done no research you have no right to say anything.Be careful for every word you utter.

TRA mtumishi wa chini gros salary 482,500/ na wajuu ni 5,755,000/ hapo ni nje ya posho zao...! Na ukifanya kaz nje ya ofisi,per day ni 15% ya salary yako! Bot mtumishi wa chini salary pamoja na allowance nyingine ni 872,500/ na wajuu ni 8,656,000/ nje ya malupulupu!

Nakuunga mkono, watu wengi hawaelewi mada na hoja za watu haraka, kosa la serikali ni kushindwa kuweka utaratibu wa mishahara kwa kada zote unaofanana. hoja hapa ingekuwa marupurupu kutokana na aina ya kazi unayofanya. Na hilo kosa ambalo ni la kibaguzi ndo linawatesa leo. Eti digrii moja ya Udaktari 960,000/- kwa mwezi, digrii hiyo hiyo ya Uhasibu 300,000/-, Sasa hiki ndo kinawatesa, mshahara ungekuwa mmoja harafu tofauti kidogo kwenye marupurupu kama on call allowance ambayo haipo kwa mhasibu n.k.

U- daktari si sawa na uhasibu , hivi ugumu na umuhimu wa science ni sawa na Uhasibu ?
hapa suala ni upate mshahara kutokana na ubora na umuhimu wa kazi yako ,

TRA mtumishi wa chini gros salary 482,500/ na wajuu ni 5,755,000/ hapo ni nje ya posho zao...! Na ukifanya kaz nje ya ofisi,per day ni 15% ya salary yako! Bot mtumishi wa chini salary pamoja na allowance nyingine ni 872,500/ na wajuu ni 8,656,000/ nje ya malupulupu!
Na mil 20 za Prof Ndullu zipo kundi gani hapo ?

Hzo scale ni za watumishi wa chini ya wakurugenzi,ktk pay roll wagukurugenzi mishahara yao imeandikwa fixed na hawajaonyesha viwango,! Hii ndio serikali ya Chukua Chako Mapema(C.C.M) inavyokwenda!

Hiyo Tsh Mil 3- 4 ni gross au net? kama ni gross , basi net ya 3m= Ths 1,994,000 , gross ya 4 = Tshs 2,624,000.

Siyo nyingi kihivyo, labda kama ndio unaanza kazi na huna majukumu.

Hiyo ni basic salary (kabla ya kukatwa PAYEE, NPF/NSSF/NHIF) na michango mingine ya kitaaluma. Kimsingi Prof. take home yake ni kati ya 1.8mln-2.5mln.

Prof. wengi wanategemea zaidi utafiti na ushauri kuwaongezea kipato.

Una uhakika na hicho unachoongea au ni redio mestini?Kama unajua mishahara ya wahadhiri imeboreshwa ebu tujuze kwa kiasi gani?Unazijua posho zinazolipwa na viongozi wastaafu wa ngazi za juu hapa nchini? If you done no research you have no right to say anything.Be careful for every word you utter.

Nina uhakika wa asilimia 110.

Back
Top Bottom