comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Mfuko wa Sekta Binafsi nchini (TPSF) umesema ujio wa viwanda 200 kutoka nchini China,Serikali inatakiwa kujipanga kupokea viwanda hivyo kwani vitachangia kukua kwa uchumi pamoja na ajira nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema China kwa sasa ni nchi yenye mitaji mikubwa kuliko nyingine duniani hivyo lazima kuongeza mahusiano zaidi ili kuweza kunemeeka nao katika kuelekea uchumi wa kati wa viwanda kufikia 2025.
Simbeye amesema viwanda vingi vya China vimefikia hatua ya kuweza kuhamishwa katika sehemu mbalimbali katika Bara la Afrika na kuendelea na uzalishaji kutokana na uhakika wa rasilimali watu pamoja na malighafi.
Amesema kutokana na uwekezaji wa viwanda hivyo suala la maeneo tengefu liangaliwe kimkakati katika kufanya maandalizi ya viwanda hivyo pamoja na vingine vitakavyojengwa.Simbeye amesema nchi ya China ina uwezo mkubwa wa mitaji kuliko maeneo mengine duniani na Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda zilizowawezesha kufanya mapinduzi ya viwanda.
Aidha amesema ujio wa Waziri wa Mambo ya Nchi wa China nchini ni sehemu ya kuchangamkia fursa kwa karibu kwa kuongeza uhusiano uzidi kudumu ambao wenye maendeleo baina ya nchi mbili.
Chanzo: ITV