TPC wagawana Sh 659 milioni bonasi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KIWANDA cha sukari cha TPC kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, kimetoa Sh 659.5 milioni kama bonasi kwa wafanyakazi wake 1,722 ikiwa ni faida iliyopatikana kwa mwaka 2009/10.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho, Robert Baissac kwa waandishi wa habari imeeleza kuwa bonasi hiyo inatokana na faida waliyoipata kwa kipindi hicho.

Alisema bonasi hiyo italipwa kwa wafanyakazi wote wanaostahili kwa mujibu wa mkataba wa hiari kati ya TPC na Chama cha Wafanyakazi wa Huduma za Kijamii na Viwanda (Tasiwu) uliotiwa saini Aprili 23, mwaka jana.

Baissac alisema katika bonasi hiyo ambayo imelipwa pamoja na mshahara wa mwezi Desemba itakatwa kodi kwa mujibu wa sheria na kila mfanyakazi atalipwa Sh,382,993 zikiwa bonasi itokanayo na faida.

Ofisa Mtendaji mkuu alisema kwa mujibu wa kifungu namba 22.0 cha mkataba kati ya Tasiwu na TPC kimeonyesha wazi kuwa faida itakayopatikana italipwa kwa wafanyakazi walioshiriki kikamilifu katika mwaka wa uzalishaji husika.

“Chini ya mkataba huo wafanyakazi wote walioshiriki kikamilifu katika uzalishaji wa mwaka wa fedha 2009/10 wanastahili kulipwa bonsai itokanayo na faida, lakini wafanyakazi waliokosa kazini bila sababu ya msingi hawatastahili kulipwa bonasi chini ya kifungu namba 22.0 cha mkataba,”alisema.


Alisema katika msimu huo kiwanda hicho kilizalisha tani 68,584 za sukari kiwango ambacho ni kidogo ikilinganishwa na msimu uliopita, lakini walipata faida nzuri kutokana na bei nzuri ya sukari iliyopatikana kwenye soko.

Kwa mujibu wa Baissac alisema bonasi iliyotolewa ni kubwa na ambayo haijawahi kulipwa na kiwanda hicho hivyo akawataka wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi kudumisha upendo ,kuaminiana kufanya kazi kwa bidii ,umakini na juhudi zaidi kwa lengo la kukuza uzalishaji wenye faida na manufaa kwa wadau wote.

Alisema faida hiyo imetokana na kufanya kazi kwa utulivu na usalama na ni vyema kudumisha mawasiliano mazuri yaliyopo na kufunga mianya ambayo inaweza kuathiri maelewano kati yao na kusababisha kuibuka kutokuelewana kati yao.
 
Hongera sana TPC. Kwa jinsi mambo yanavyokwenda, you have done wonderful job. Viwanda vya Tanzania karibu vyote vimekufa au viko hoi bin taabani. Manufacturing na agro processing lazima wafufue upya.
 
If people are good only because they fear punishment, and hope for reward, then we are a sorry lot indeed.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom