TPA yapokea msaada wa dola za Marekani milioni 60 kwa ajili ya miradi ya bandari

TPA

Member
Sep 28, 2016
49
71
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeingia makubaliano na Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) ambayo itatoa msaada wenye thamani ya Dola Marekani Milioni 60 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 132 kwa ajili ya maboresho ya miradi mbalimbali ya Bandari ya Dar es Salaam.

Msaada huo unatarajiwa kusaidia uboreshaji wa barabara za ndani ya bandari, eneo la uhifadhi wa makontena, mizigo, kuongeza uwezo wa bandari kuchukua meli kubwa zaidi, kuendesha upembuzi yakinifu wa kuanisha maeneo mengine ya maboresho, kuifanya bandari ya Dar es Salaam kuwa rafiki ‘green port’ na kuangalia maboresho zaidi ya mifumo ya kielektroniki.

Makubaliano hayo yamefanyika leo Makao Makuu ya Mamlaka ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga walitia saini makubaliano hayo mbele ya vyombo vya habari.




Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (watatu kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga (wapili kulia) wakiweka saini makubaliano hayo mbele ya vyombo vya habari



Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko akibadilishana hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga mara baada ya kuweka saini makubaliano hayo.



Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko na Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga wakionesha hati ya makubaliano mara baada ya kuweka saini makubaliano hayo.




Mkuu wa Shirika la DFID Tanzania, Bw. Vel Gnanendran (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo. Katikati ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Karim Mattaka.



Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (wanne kushoto) akijibu maswali ya waandishi wa habari katika hafla hiyo.



Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga (kulia) akijibu maswali ya waandishi wa habari katika hafla hiyo.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakishuhudua tukio hilo.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakishuhudua tukio hilo.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakishuhudua tukio hilo.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakishuhudua tukio hilo.
 
Mkuu TPA, kwanza nimefarijika sana kuwa ni mmoja miongoni mwa walioshuhudia tukio hili jana hapo makao makuu ya TPA, nimefarijika zaidi kujua TPA ni member wa jf, hivyo sasa jf tutakuwa tunapata reliable info kutoka bandarini, hii itaisaidia sana jf kupata info za uhakika, big up TPA ku join JF.

Sahihisho dogo, Trademark East Africa sio kampuni, ni taasisi ambayo ni NGO.

Paskali
 
Naona DG wa TPA ex-Tanroads anajaribu kuisogeza mbele bandari yetu. Safi sana Engineer!
 
Reactions: TPA
Hongereni sana TPA,Naomba sana muangalie miundo mbinu ya getini hasa wakati wakutoa mizigo mipana na mikubwa sisi watu wa usafirishaji tunapata shoda sana kona ni ndogo sana hasa geti no 3,jaribuni kuliangalia upya bado mageti yenu niyale ya zamani,kuweka hizo mashine za ukaguzi sio suluwisho kikubwa nikuweka njia pana na bora ya kupitisha kila aina ya mizgo.Muangalie na SCANA mashine utendaji sio mzuri wa hapo ni hatari sana kwa maisha ya madereva
 
Reactions: TPA

Asante Pascal tumesharekebisha.
 

Steven tunashukuru ushauri wako utafanyiwa kazi.
 
mnaboresha ili mtoe mizigo gani au baada ya miaka 10 ?
 
Mkuu hujajibu swali, tofauti ya msaada na mkopo? maanake kila siku nasikia misaada lakini deni la taifa linaongezekana.
Umeshaambiwa ni msaada wewe unang'ang'ania mkpo sijui deni la taifa linaongezeka. TPA haiwezi kuongelea deni la taifa hilo muulize waziri wa fedha ila naona tpa wapo clear kwamba ni msaada kutoka uingereza
 
Umeshaambiwa ni msaada wewe unang'ang'ania mkpo sijui deni la taifa linaongezeka. TPA haiwezi kuongelea deni la taifa hilo muulize waziri wa fedha ila naona tpa wapo clear kwamba ni msaada kutoka uingereza
Hujalazimishwa kujibu, acha wajibu wenye ufahamu. Tatizo nini kwako?
 
it's shameful kwa taasisi kama TPA kusaidiwa. operations zake ni 100% commercial oriented so ina uwezo wote kabisa wa kuji-sustain yenyewe.

misaada kama hii is nothing to be proud of at all.

hospitali zetu zinahitaji madawa na vifaa. elekezeni huu umatonya kule at least.
 
Kuna makubaliano wamefanya kwa mujibu wa taarifa hiyo! Hakuna msaada ulio na makubaliano! Makubaliano ~ Masharti
 
Tukizoea kuomba omba kuna siku TPA wataomba bahari kutoka USA..maji yapo tuu hayo punguzeni figisu figisu na kodi mizigo ije mingi muweze kujiendesha wenyewe bila kutegemea misaada kila kukicha na huku uwezo tunao...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…