TPA yakiri kupungua kwa shehena ya makontena Bandarini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Habari wanaJF,

Hatimae mamlaka ya bandari ya Tanzania yaani TPA leo jumatatu tarehe 02.05.2016 wamejitokeza hadharani na kukiri kupungua kwa mizigo inayoingia kupitia bandari haswa ya Dar es Salaam.

leaders.jpg

Wakiongea na waandishi wa habari maafisa wa TPA wasemesema sababu kubwa kuwa ni uchumi wa dunia kuyumba na haswa nchi kama China na kwingineko ambako mizigo inayopitia bandari ya Dar es Saam hutoka.

===========

My Take: Isijekuwa hii sio sababu thabiti yawezekana yapo mengi nyuma ya pazia
 
My take: Isijekuwa hii sio sababu thabiti yawezekana yapo mengi nyuma ya pazia
Wale waliokuwa wanaleta makontena meeengi bila kulipia au kulipia kiduchu sasa hivi wamepunguza au hawaleti kabisa. Afadhali machache yanayolipiwa ipasavyo kuliko mengi yasiyolipiwa.
 
Wale waliokuwa wanaleta makontena meeengi bila kulipia au kulipia kiduchu sasa hivi wamepunguza au hawaleti kabisa. Afadhali machache yanayolipiwa ipasavyo kuliko mengi yasiyolipiwa.
N aya magumashi yakipungua, hata ya halali process ya kuyaondoa bandari inakuwa ya kasi zaidi
 
Na ndo maana vitu vinapanda bei, sababu inaonekana supply inapungua. Swala kwamba kushuka kwa uchumi wa dunia ndo kumesababisha kushuka kwa kuingizwa bidhaa sio kweli kabisa, sasaiv nchi nyingi interest rate iko chini sana, kwa mfano japan nadhan ni negative kabisa, maana yake kuweka hela benki ni gharama kuliko kuwa nazo, lengo ni ku encourage spending. Sis kama waagizaj wapo bidhaa huko duniani zinatafuta watu, isipokuwa sis tuna magumashi yetu tu tukubali. Ndo maana tumeanza kukwama.
 
Wale waliokuwa wanaleta makontena meeengi bila kulipia au kulipia kiduchu sasa hivi wamepunguza au hawaleti kabisa. Afadhali machache yanayolipiwa ipasavyo kuliko mengi yasiyolipiwa.

umenena vyema na ndiyo maana mapato ya forodha pamoja na uchache wa macontainer lakini hayajashuka below 100% mpaka sasa. Bora machache yanayolipa kodi kuliko msongamano wa macontainer ya wakwepa kodi.
 
Ukweli ni kuwa biashara huku mtaani zinastruggle kutokana na Wanunuzi kutokuwepo...Wanunuzi hawapo kwa sababu ya hali ngumu ya maisha ...inflation iko juu na Purchasing Power inazidi kushuka.......

Kwa hiyo kama demand ime fall drastically usitegemee kuwa Imports zitaongezeka....zitashuka......na hiyo ndiyo sababu ya wafanyabiashara kutoagiza bidhaa kipindi hiki

Pia ikumbukwe huu sio msimu wa mavuno kwa hiyo hata pesa imepungua kwenye mzunguko
 
Ukawa wanaona ni faida sana kuwa na mizigo mingi isiyolipiwa kodi kuliko kua na mizigo michache inayolipiwa kodi ipasavyo.

huelewi root cause wewe .....Ishu sio hiyo...Ishu ni Raising inflation ..na kushuka kwa purchasing power...Demand imeshuka....kwa hiyo wafanyabiashara hawawezi ku import
 
Juzi wakati hizi taarifa zinatoka ccm walisema si za kweli na ni uongo wa mafisadi waliokuwa wanapitisha mizigo bila kulipia..

Naomba mjitokeze leo kupinga kauli hii.
Kwani ni lazima kuchomekea Siasa kwenye kila kitu?????????
 
huelewi root cause wewe .....Ishu sio hiyo...Ishu ni Raising inflation ..na kushuka kwa purchasing power...Demand imeshuka....kwa hiyo wafanyabiashara hawawezi ku import
Umeshaambiwa hapo sababu ni kuyumba kwa uchumi wa dunia hasa hasa china ambako mizigo mingi hutoka, sasa mkuu naona wewe umekomalia hapa nyumbani pekee, we do not live in isolation kama huko duniani na hasa kwa wakubwa hali ni tete, hata sisi pia tunapata madhara kama hivi..
 
mizigo mingi sasa hivi mambo yote ni Beira au Mombasa au Durban.

watu wamechoka na uswahili wa Kikwere/Kisukuma/ etc!!
 
Habari wanaJF,

Hatimae mamlaka ya bandari ya Tanzania yaani TPA leo jumatatu tarehe 02.05.2016 wamejitokeza hadharani na kukiri kupungua kwa mizigo inayoingia kupitia bandari haswa ya Dar es Salaam.

View attachment 344127

Wakiongea na waandishi wa habari maafisa wa TPA wasemesema sababu kubwa kuwa ni uchumi wa dunia kuyumba na haswa nchi kama China na kwingineko ambako mizigo inayopitia bandari ya Dar es Saam hutoka.

===========

My Take: Isijekuwa hii sio sababu thabiti yawezekana yapo mengi nyuma ya pazia
Mkuu amesahau kutujulisha ni mizigo ipi imepunguka. Ni internal au transit goods?
 
Sababu za kweli ni hizi hawataki kusema ;
1. Kukamilika kwa ujenzi wa Bandari ya Beira Msumbiji pamoja na kukamilika kwa Reli ya Malawi to Beira , so Mzigo wa Malawi uliokuwa unapitia Dar sasa unapitia Beira , pamoja na Mzigo kutoka Zambia kupitia bandari hiyo.

2. Mizigo ya Mashariki ya Congo , kwa sababu za kisiasa JK alikubaliana na Kabila kuwa kodi yote itozwe Bandari ya DSM , sasa mtaelewa nchi iliyoko vitani kodi ni hadithi sasa nani akubali ? wamehamia bandari ya Durban South Africa.
3. Bandari ya DSM inatoza kodi kwa dola wakati ile ya Durban inatoza kwa Rand , kitu ambacho kinawapa unafuu wa kodi kutokana na thamani ya rand kushuka ukilinganisha na Dola.
4. Wafanyabiashara wa ndani wanashindwa kuagiza mizigo kutokana na mfumo wetu wa kodi kuwa wa kukadiria baada ya mzigo kufika na hakuna kipimo chochote cha kisayansi cha makadirio hayo, hivyo kujikuta wanapata hasara zaidi. Mf,unaagiza gari kutoka Japan kwa bei ya dola 2,800 lakini TRA wanakataa kuwa hakuna bei ya gari ya aina hiyo pamoja na ukiwa na nyaraka zote hawajali wanakukadiria wao kinyume na bei halisi , hapa wanafanya ili kuongeza mapato waonekane wamekusanya kupita lengo , so wamevuta pumzi ya kuagiza.Hata kwenye maduka Kariakoo wanachajiwa juu sana sasa wanapata hasara wakiuza kwa sababu bei ya soko hailingani na kiwango cha uwezo wa kununua.

Watangaze Makusanyo ya mwezi Aprili ndio mtajua ninachosema .......Mzigo umepungua by 60% hata Copper iliyokuwa inapita kutokea Zambia inapitia Durban .......mwenye muda fuatilia ufanisi wa mizigo bandari ya Durban tangu January 2016 check mzigo wa Zambia ni asilimia ngapi.
 
Kule Mtwara mdau wangu ananitonya kuwa tangu mwezi January, bandari iko empty, kama ni kweli juhudi za makusudi zifanyike kunusuru!
 
Back
Top Bottom