Tozo kwenye miamala na mabenki ni rahisi kukusanywa lakini hazina tija Kwa serikali

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Bado naweka argument yangu kuwa vyanzo vyote vya mapato ambavyo serikali ni mlipaji mkuu havina tija ingawa kwenye takwimu kuna sekta zitajisifu...

1.Tozo kwenye Miamala, uwekaji na utoaji fedha benki, serikali ndiyo mlipaji mkuu maana matrilioni ya fedha Kwa maendeleo na matumizi yapo benki na hata fedha za misaada na kandarasi zote zipo benki hii ina maana serikali Inatoa fedha mfuko Wa nyuma inaweka mfuko Wa mbele halafu tunasema mapato yameongezeka.

2.Serikali inanunua vichwa vya treni, vifaa vya ujenzi Wa reli na hata Bwawa la umeme nk na kulipa kodi kubwa kutokana na gharama zake...

TRA wanatangaza kuvuka malengo ya ukusanyaji kumbe fedha imetolewa mfuko Wa nyuma Inawekwa mfuko Wa mbele.

Kodi na tozo aina hizi zinaonesha serikali Imekusanya mapato makubwa lakini unashangaa Kwa nini Inapata ugumu Wa kutekeleza mipango yake.
 
Tozo ni kodi kwa maskini tu maana hakuna tajiri anafanya miamala kwa njia ya simu
 
Samia anaupigi mwingi hadi anachana nyavu

Nakumbushia tu, tambo za miezi kadhaa iliyopita
 
Back
Top Bottom