Toyota Vitz 2005 990cc vs 1290cc

Banned

Member
Apr 7, 2013
45
12
Habari wakuu!
Mimi ni mgeni kwenye haya maswala ya magari na nilitaka nitolewe tongotongo! Kuna hizi Vitz muundo mpya wa kuanzia 2005 nilitaka kujua uwezo wake kwa mizunguko ya hapa DSM na ulaji wake wa mafuta na uwezo wake labda kusogea kidogo mpaka Mkoa wa Pwani au mara chache Morogoro. Je, zinaweza kustahimili au ndo kuchemsha kama nilivosoma kwenye thread moja kuhusu Toyota Passo!

Maelezo ya ziada ya gari
zipo Vitz za >2005 zenye 990cc na zina engine code 1KR na nyingine ni 1290cc either engine code 2NZ au ipo yenye engine code 2SZ!

Budget yake kutoka Japan ni around 9.3M kupanda juu na iko ndani ya budget yangu je nichague ipi kati ya hizo kulingana na hayo matumizi yangu na ulaji wa mafuta!

BF696227_79894f.jpg

Shukrani!
 
Kwanza kabisa hilo suala la Passo sijui kuchemsha ni uvumi unaoenezwa na watu wachache wanaojifanya wana "MAGARI".

Swali la kujiuliza, hizo Passo zipo Arusha au Songea, zilibebwa au? Zilitembea.
Kumbe safari zinavumilia ila sio za mara kwa mara.

Mie kwa Ushauri naona bora uchukue Vitz RS ya Engine ya 1.3 L 2SZ-FE I4 ya 2005. Ni Sport version, nyepesi kuchanganya, mwendo upo na ni imara sana.

Hizo unazozisema sio imara sana. Hasa bodi yake naona kwa barabara zetu sio nzuri sana. Hii naisemea kwa Experience, ya kwangu ni kama hiyo ya 2005, namba ni BLZ na nilinunua kwa mtu hapa hapa Bongo.

Ila imeshapiga trip za Dar-Kigoma-Dar, Dar-Mwanza-Dar x2, Dar-Arusha-Dar, na Dar-Mbeya-Dar.

Sijagusa engine zaidi ya service za kawaida tu na tyre kubadilisha. Nimebadili shock absorber mara moja.

So mie binafsi kwa ushauri naona VITZ RS ya 2005 inajitahidi sana kwa uimara
 
Namuunga mkono Prince .

Chukua ya 1.3. Hiyo 990cc litakuwa zito sana. Mtakuwa pamoja na Bajaji kwenye tuta, utaona anakuovertake kama umesimama vile. Tho kwa mafuta uta enjoy sana.

Nina mshokaji alikuwa na Passo ya 990cc duh... Jamaa alikuwa anapiga misele town mafuta ya elfu 20 mpaka anasahau aliweka lini mafuta. Kama wewe sio mzee kwa kushindana na watu chukua la 990cc.

Litafika mikoani, muhimu service na pia usishindane na ma V8 utakayo yaona. Nenda mwendo wa pole pole, kwani ni Salama kwa maisha yako, engine yako na pia mafuta utakuwa unatumia kidogo. Why? Gari kama Passo ukiwa unatembea na 100kmph na Brevis ukiwa unatembea the same speed. Passo litakula mafuta kuliko Brevis. In short tembea na Mwendo unaoendana na engine yako utafika Salama salmin.

Good luck

-callmeGhost
 
passo... kama huna haraka sana barabara kuu, hupendi speed, ni muumini wa polepole ndiyo mwendo.. una weza vumilia ukiona mtu wa bajaji anakupita. pia huna uzito mkubwa wewe na mkeo au mwanao au wanao kwa maana ya kuwa msije mkawa wazito ikifika kwenye mlima inabidi mshuke gari ipande au inadibi kusukuma wakati flan.

jitahidi uwe unaishi sehemu ambayo ni tambalale. pia zingatia vigezo vya uzito. kama una marafiki wabonge , au ndugu zako halaf wakaomba uwapeleke sehemu... usikubali gari linaweza kukuaibisha. kifupi ukiwa na passo ni sawa na kuwa na bajaji sema hii passo unakuwa upo kwa ndani na ni miguu 4. mimi binafsi huwa nachukulia hivi vigari ni kama vilitengenezwa na wanafunzi waliokuwa field huko japani kwa ajili ya kuwasaidias watoto wadogo na wadada wa kazi wanapoenda sokoni kununua bidhaa za matumizi home.

na kwa nini uitese gari yako kuipeleka mbeya,iringa n.k ? kwa nini uwe na ukatili kiasi hicho? no si vema tuwe na huruma na hivi viumbe.gari nazo zina hisia na unawea kuta inanung'unika sana unapoifanyisha kazi isizoziweza. kama vipi si ununue gari angalau ya kuanzia cc 2000? si mbaya kama hizi za cc 3000 na kuendelea unaona hazikufai. nunua hata rav 4 na ndugu zake. achana na hako kadude..katakukera tu ndugu yangu.
 
passo... kama huna haraka sana barabara kuu, hupendi speed, ni muumini wa polepole ndiyo mwendo.. una weza vumilia ukiona mtu wa bajaji anakupita. pia huna uzito mkubwa wewe na mkeo au mwanao au wanao kwa maana ya kuwa msije mkawa wazito ikifika kwenye mlima inabidi mshuke gari ipande au inadibi kusukuma wakati flan. jitahidi uwe unaishi sehemu ambayo ni tambalale. pia zingatia vigezo vya uzito. kama una marafiki wabonge , au ndugu zako halaf wakaomba uwapeleke sehemu... usikubali gari linaweza kukuaibisha. kifupi ukiwa na passo ni sawa na kuwa na bajaji sema hii passo unakuwa upo kwa ndani na ni miguu 4. mimi binafsi huwa nachukulia hivi vigari ni kama vilitengenezwa na wanafunzi waliokuwa field huko japani kwa ajili ya kuwasaidias watoto wadogo na wadada wa kazi wanapoenda sokoni kununua bidhaa za matumizi home.

asante Mkuu kwa mchango wako japo mjadala umejikita kwenye Passo kuzidi Vitz mbili zilizotajwa!
ila pia budget yangu pia nilionesha kwenye thread hapo juu natamani hayo makubwa zaidi ila ndo hivo tena!
 
passo... kama huna haraka sana barabara kuu, hupendi speed, ni muumini wa polepole ndiyo mwendo.. una weza vumilia ukiona mtu wa bajaji anakupita. pia huna uzito mkubwa wewe na mkeo au mwanao au wanao kwa maana ya kuwa msije mkawa wazito ikifika kwenye mlima inabidi mshuke gari ipande au inadibi kusukuma wakati flan. jitahidi uwe unaishi sehemu ambayo ni tambalale. pia zingatia vigezo vya uzito. kama una marafiki wabonge , au ndugu zako halaf wakaomba uwapeleke sehemu... usikubali gari linaweza kukuaibisha. kifupi ukiwa na passo ni sawa na kuwa na bajaji sema hii passo unakuwa upo kwa ndani na ni miguu 4. mimi binafsi huwa nachukulia hivi vigari ni kama vilitengenezwa na wanafunzi waliokuwa field huko japani kwa ajili ya kuwasaidias watoto wadogo na wadada wa kazi wanapoenda sokoni kununua bidhaa za matumizi home.

na kwa nini uitese gari yako kuipeleka mbeya,iringa n.k ? kwa nini uwe na ukatili kiasi hicho? no si vema tuwe na huruma na hivi viumbe.gari nazo zina hisia na unawea kuta inanung'unika sana unapoifanyisha kazi isizoziweza. kama vipi si ununue gari angalau ya kuanzia cc 2000? si mbaya kama hizi za cc 3000 na kuendelea unaona hazikufai. nunua hata rav 4 na ndugu zake. achana na hako kadude..katakukera tu ndugu yangu.
Kha mkuu asante sana nimecheka kwa haya majungu
 
Back
Top Bottom