Mkuu Wangu alinunua prado 00km, mwaka 2014, leo inazaidi ya km 200,000 lakini gari haina hata shida, na inakwenda mikoa kila leo..Binafsi naona kuwa gari regardless imetembea km ngapi, kama unaifanyia haki kwenye service na machine (engine) bado iko vizuri, kwa maana ya kuwa bado ina nguvu, shock ups na tyre ziko vizuri pamoja na transmission, you can go anywhere.
Mfano mie nina Honda CRV imetembea km 180000+ ila juzi nimeenda nayo Musoma na kurudi Iringa bila shida. Gari nilinunua 2011. Kikubwa ni matunzo tu kwenye gari